Kusafisha na kung'arisha uso vizuri, tumia face wash au facial cleanser

Kusafisha na kung'arisha uso vizuri, tumia face wash au facial cleanser

Magnificient

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
1,162
Reaction score
705
UTUMIAJI WA FACE WASH AU FACIAL CLEANSERS HUPENDEZESHA ZAIDI USO WAKO
U hali gani rafiki yetu na mpenzi wa mambo ya vipodozi na muonekano wa mwili? Karibu katika somo la leo linalohusiana na vipodozi viitwavyo Face Wash au Facial Cleanser vitumikavyo kwa ajili ya kuoshea uso.

FACE WASH/FACIAL CLEANSER NI NINI?

Face wash au Facial cleanser ni vipodozi vinavyofanya kazi ya kusafisha uso kwa kiasi kikubwa kabisa kwa kuyayusha na kuondoa kiasi kikubwa cha uchafu wa usoni kama vile mafuta, jasho, vumbi, seli zilizokufa na takataka zingine.
Matokeo yake ni kwamba mtu ambaye ametumia kipodozi hiki anabaki na ngozi safi kabisa na inayong’aa kwa sababu kiasi kikubwa sana cha uchafu na vitu vingine vilivyokuwa vinafunika ngozi yake vimeondolewa. Ufanisi wake katika kusafisha uso ni mkubwa kuliko sabuni.

KWA NINI NI BORA UKATUMIA FACE WASH AU FACIAL CLEANSER?

Kwanza Face wash au Facial cleanser zinasaidia kuondoa sehemu kubwa sana ya uchafu na vitu vingine vinavyoziba ngozi yako. Hii ni bora zaidi kwa sababu itakuacha na ngozi laini, inayong’aa na kuvutia vizuri.
Pili Face wash sio kali sana kama sabuni, na ni nzuri zaidi kuoshea uso wako. Sabuni huweza kuwa kali na pia kama ni ya mche au kipande huweza kuwa inaharibu ngozi yako na kupasua chunusi, kuleta michubuko nk kama utajisugulia kwa nguvu.
Hayo hufanya Face wash au Facial Cleansers kuwa bora zaidi katika kusaidia kuondoa chunusi na pimples, kung’arisha uso, kumaliza uchafu usoni, kuzuia magonjwa ya ngozi usoni, kupunguza kasi ya uso kuzeeka na kuzipa seli za uso kuweza kupumua, kukua na kuendelea vizuri.

MAMBO YA KUZINGATIA

Chagua Face Wash/Facial Cleanser nzuri na yenye ubora unaofaa kwa ngozi yako. Kama ngozi yako ni kavu chagua Face wash kwa ajili ya ngozi kavu, na kama uso wako ni wa mafuta basi chagua face wash/facial cleanser kwa ajili ya uso wa mafuta. Kadhalika na kwa ngozi ya kawaida na ngozi mchanganyiko.
Tafuta ya gharama unayoimudu vizuri ili uweze kuitumia vizuri na kwa uhuru zaidi.
Kuna Face wash/Facial Cleanser zinazoweza kuwa feki na kali kwa ngozi yako. Pata ushauri kutoka kwa watu wanaojua vizuri masuala ya vipodozi na uzuri wa mwili.
S&E BEAUTY SOLUTIONS inakutakia kila la kheri katika kujipendezesha na uzuri wako.
Kama una tatizo lolote , swali au unahitaji bidhaa yoyote au ushauri wa afya, urembo na vipodozi karibu sana.
 
Asante kwa mada nzur...Hii face wash ni kwa kina dada tu au na wanaume? Ina tofauti gani na scrub?
Face wash ni kwa ajili ya watu wote, wanawake na wanaume. Ila kuna baadhi yao zipo mahususi kwa jinsia ya kike au ya kiume, na utakuta zimeandikwa kabisa. Kwa mfano NIVEA FACIAL CLEANSER FOR MEN.

Facial Cleanser na Scrub zina tofauti. Scrub kazi yake ni kuondoa seli za ngozi ya nje kabisa ambazo zimekufa na kuifanya ngozi kufubaa, ila Facial Cleanser hufanya kazi ya kusafisha na kuondoa uchafu wowote ambao hubaki kwenye ngozi - mafuta, vumbi, wadudu, seli zilizokufa na.

Unashauriwa kutumia scrub mara 1 mpaka 2 kwa wiki, lakini face wash unaweza kutumia kila siku.
Vyote vitaufanya uso wako kung'aa na kupendeza.
 
Asante kwa maelezo mazuri nitapita leo dukani nikachukue, hope hii nitakuwa naipaka usoni tu tena kama mafuta ya kawaida au nahitaji kupaka kwa kusugua sugua uso? Ipi ni brand nzuri? Una maelezo yoyote ya ziada? Nashukuru.
 
Asante kwa maelezo mazuri nitapita leo dukani nikachukue, hope hii nitakuwa naipaka usoni tu tena kama mafuta ya kawaida au nahitaji kupaka kwa kusugua sugua uso? Ipi ni brand nzuri? Una maelezo yoyote ya ziada? Nashukuru
Ni vyema kuiosha kwa maji baada ya kuitumia, usiiache usoni kama mafuta au lotion; itumie kama sabuni ya maji. Brand zipo za aina nyingi kama vile za NIVEA, BRILLARE, APRICOT, VASELINE na kadhalika. Zitafute Pharmacy, Supermarkets na maduka ya vipodozi yanayouza vipodozi vizuri.
 
Ndugu Magnificent hongera sana kwa mada nzuri.
Mimi ngoja nichangie kwa uzoefu wangu ambao nimeifunza kupitia mawazo ya watu kama nyie.

Mimi huwa nina ratiba kabisa ambayo nimeiweka kwenye board. Hii hunisaidia kuniguide kila siku ni nini natakiwa kufanya kwa uso wangu bila kupoteza muda. Ukweli nimepata mafanikio sana na pia imenifanya nione ni kitu rahisi sana. Ratiba ipo kama ifuatavyo:

Jumatatu- 1.sabuni kawaida 2. facewash(cleancer): vyote tumia kitambaa laini
Jumanne- 1.sabuni kawaida kwa kutumia dodoki (ila hutumii nguvu). Mi natumia haya madodoki ya kienyeji kwani ni mazuri sana.
Jumatano-1.sabuni kawaida 2. scrub: vyote tumia kitambaa laini
Alhamis-1.sabuni kawaida 2. facewash(cleancer): vyote tumia kitambaa laini
Ijumaa- 1.sabuni kawaida kwa kutumia dodoki
Jumamosi-1.sabuni kawaida 2. scrub: vyote tumia kitambaa laini
jumapili-1.sabuni kawaida 2. facewash(cleancer): vyote tumia kitambaa laini

MUHIM: Paka sabuni kias(unayotumia siku zote) kwenye kitambaa kilicho na unyevu halafu jisafishe taratibu. kisha nawa vizuri kutoa sabuni na pia kitambaa chako kisafishe. Halafu paka face wash yako kidogo tu kwenye kitambaa hichohicho chenye unyevu na usafishe tena taratibu uso wako. kila kitendo ni kama dakika mbili tu inatosha. Ukimaliza safisa vyema face wash usoni kwa maji safi. Baada ya hapo endelea na kuoga mwili wote. Kwa sasa nimegundua aina flani ya soksi za cotton ambazo zinatexture nzuri sana kwa kusafishia uso. Ni muhim sana usitumie nguvu nyingi kwenye kusafisha uso maana ngozi itachoka mapema. Fanya kama unamuogesha mtoto mchanga kabisaaa. Hili ni muhim kuzingatia.

Baada ya kumaliza kujisafisha ni muhim kupaka kwanza "tonner" halafu fuatia moisturizer au mafuta/lotion uliyozoea. Ukifata vyema utaratibu huu itasaidia kuboresha ngozi yako ya uso. Ila msiache kunywa maji hasa asubuhi kabla ya kunywa chai. Unaweza kutumia mavipodozi ya gharama ila kama huli vizuri na kunywa maji ya kutosha vitadunda tu!!
 
tonner ndo nini?
 
Back
Top Bottom