Kusaidia Ndugu/familia ni wajibu au lazima?

Ungewaambia waache ungese wao.
 
Ubinafsi si mzuri kama una nafasi au kipato saidia tu wenye uhitaji kwa kufanya hivyo unajenga koo au familia yenye nguvu kiuchumi na maamuzi ktk jamii
Swali langu ni kwamba wakati mimi napambana wao walikua wanafanya nini!?

mana hapa naona tunapeana ulemavu na ufukara.

nadhani ni vema kubadili mifumo ya maisha yetu kuiboresha mara mbili Au zaidi ya tulipotoka.

leo hii siwezi ona mtoto wangu aje kusomeshwa na mtu.

lengo ni kurithisha uwezo mbele zaidi.
Tuache hizi style za kizee.
 
Kwa andiko hili naamini wewe ni mcha Mungu na bila shaka ni mtu mwenye mafanikio. What a great thinker! Thanks.
Hapa pia kuna tatizo.

ata imani ilisema asiyefanya kazi na asile.

lengo langu ni kizazi chetu nije kurithisha mafaniko sio shida.

mtegemea cha ndugu hufa maskini.

kusaidia kusiwe sababu ya kisingizio cha kutofanikiwa.

kuamini Mungu ni imani ya mtu.
(With respect)

lakiki tukitumia vibaya imani pia inaleta chanzo cha ufukara.
 
Ubinafsi si mzuri kama una nafasi au kipato saidia tu wenye uhitaji kwa kufanya hivyo unajenga koo au familia yenye nguvu kiuchumi na maamuzi ktk jamii
Ukijaribu kutazama kwa ukaribu
Siri mojawapo ya mafanikio ni UBINAFSI.

Hata mti uweze kwenda juu zaidi unahitaji ukate baadhi ya matawi.

Kama kipato chako kinamzigo wa kuhudumia wengine na bado hakikutoshi
You are a definition of “LOOSER”
 
Kusaidiana kupo lakini isiwe wao wanaweka vijambio chini wakisubiria misaada toka kwa wengine.
Maisha ni kupambana sio kukaa kikhanithi mwisho wa siku unaanza kulaumu ndugu yako kuwa hakusaidii.
😂😂 well said.
 
Forget history
Maisha ya sasa yanaruhusu vipi!?

kwanza hizi connection unataja sio za haki mara zote. Most likely ni kupeana priority in a shortcut way.

Hoja yangu sio kupunguza upendo “NO”

Sababu moja wapo ya kurudishana nyuma ni familia/ndugu kubweteka kwa kutegemea mwingine.

Umenisoma!?
 
Nimekuelewa sana tu

Basi kwa kujazia...kama mtu umefika ulipofika kwa msaada wa watu kadhaa, yakupasa na wewe kuwasaidia wenye uhitaji wa kweli. Sisupport wanaobweteka lakini na wewe play a certain role in someones life. Kama unaweza kusaidia hata wasiokuhusu do it.....

Nweiz kila mtu anaweza simamia anachoona kinafaa. Bless you all
 
Ndugu ni baba mama mwanao, na kaka au dada uliozaliwa nao tumbo moja... Hao wengine ni wajinga kama wajinga wengine huna haja ya kuwasaidia hata wakiumwa mahutut...
 
Anawasambaza kama boda la DHL🤣🤣
 
Kwenye suala kama hiliinategemea na familia.
Kama wewe familia ilikuchangia kukusomesha mpaka unapata kazi , hivyo nawe lazma tu utajikuta upo kwenye hako kamfumo na kwa sababu ulisaidiwa nawe saidia kama uwezo unao.
Ila kuna familia nyingine kila mtu na kafamilia kake (nucleur family base) kila mtu na habar zake , tukutane kwenye matukio ya kijamii tu .
Na mara nyingi mifumo kubadilika ni ngumu sana , sasa inategemea umekualia katka mfumo gani .
Ila suala jingine kama una uwezo wa kumsaidia mtu msaidie tu kama huna basi .
 
Inategemea umetoka familia gani, hizi familia zetu mzazi unakuta mjasiliamali mdogo hana kipato kikubwa,mzazi anakusomesha kwa tabu we na wadogo zako, bahati nzuri wewe umetoboa mzazi kazeeka hana nguvu za kutafuta hela kama zamani, wewe kama mtoto huo ni wajibu wako kumsaidia mzazi wako na wadogo zako bila kusahau kumtunza mzazi wako kwani unaweza ukakuta hana bima ya Afya. Haya ndio maisha ya watoto wengi walitoboa kutoka familia duni.

Ila kama familia bora hela yako fanyia mambo yako binafsi.
 
Acha choyo naimani na ww umepita hizo njia pia na ww kuna kipind huenda ulionekana kero kuomba omba lkn huenda ulisaidiwa usiwe na roho ya kukunja mzee saidia pale unapoweza na sio ujione umeshamaliza mwendo
 
Siku hizi nikisikia mtu anasema hasaidii mtu huwa namuelewa sana binafsi dingi yangu alikuwa first born na alisaidia wadogo zake wote almost 8 na ndugu wapembeni lakini baada ya kifo chake hakuna hata mmoja aliyetupa msaada hata katika nyakati ngumu tulizopitia.
 
Kama walikusomesha kwa kujinyima, itabidi nawe ujinyime ili usaidie kwa kadiri ya uwezo wako. Ila chunga wema usizidi uwezo.
 
Sawa ila angalia walio kunyanyua kwani uliyetafuta naye kuni ndiye wakuota nae moto.
 
Tataizo kubwa na chanzo cha haya yote ni umaskini
 
Familia zetu za Kitanazania nyingi ni maskini ! Kwa hiyo kama unao uwezo wa kusaidia hasa upande wa elimu usisite kufanya hivyo ili kuongeza wasomi watika ukoo wenu. Mungu akusaidie ili uweze kulitambia hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…