Kusajili gazeti

che wa Tz

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2011
Posts
277
Reaction score
71
Wadau naomba kuwasilisha kwenu maombi ya msaada wa kujua hatua za kusajili gazeti na mahitaji yake. Asanteni
 
unatakiwa uanzie pale posta( habari maelezo) kuna karatasi za kujaza halafu utaandika barua ya kuomba kulisajili gazeti,
ukishaipeleka ile barua wataangalia kama jina halipo halafu utapewa karatasi nyingine za kujaza hizo karatasi ndio mambo zenyewe unatakiwa
1. kuwa na mhariri mmoja
2. waandishi wa habari 4 wanaotoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali ( Tumaini dar, STJ na SAUT)
3. uthibitsho kutoka kwa printer
4. bank statement inayoonyesha fedha yenye uwezo wa kuprint gazeti mara 10 mfululizo bila kukoma

vingine vya kawaida sana ila ambavyo ni muhimu ni hivyo
 
4. bank statement inayoonyesha fedha yenye uwezo wa kuprint gazeti mara 10 mfululizo bila kukoma

vingine vya kawaida sana ila ambavyo ni muhimu ni hivyo

Hiyo bank statement inatakiwa iwe na pesa kiasi gani ambayo utaweza ku print gazet mara 10?
 
depend na aina ya gazeti unayotaka kutoa kama printer ataandika milioni moja kila toleo ina maana ni milioni 10 na kama ni milioni 6 kwa kila toleo inamaanisha ni milioni 60
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…