Kusajili LTD Company

madigida

Member
Joined
Jan 30, 2013
Posts
40
Reaction score
2
Habari zenu wana JF, nakuja leo tena naomba msaada nahitaji kufahamu taratibu na gharama za kusajili kampuni Brela.
Makao yangu ni Tanga mjini. Ninataka kuanzisha kampuni itakayo fanya shughuli za kilimo cha mboga mboga na ufungaji wa kuku wa kienyeji. Karibuni
 
Habari mudau,

Labda nianze na swali, kwani lazima iwe limited? Maana unaweza kuanza kama Sole Proprietor then baadae mtaji ukikua ndipo una ifanya Kuwa Ltd maana Ltd ni gharama na pia ina mlolongo mwingi.
1. Una propose majina matatu ili u search kule Brela, unaweza kuserach online na hata form zote unapata katika website yao.

2. Ukipata jina mwanasheria au mwenyewe unaanda Memorandum then unairudisha Brela kulipia usajiri ili upate Certificate of Incoporation ambayo inaweza kukugarimi kutokana na Kiwango cha mtaji wako katika hiyo memorundum ila Mara nyingi si chini ya laki Tatu.

3. Ukiisha pata Cert of Incorp unaenda TRA kuprocess TIN ya kampuni pamoja na wakurugenzi wake ni bure.

4.Ukiishapata TIN ndo unaenda manispaa kuomba leseni ya bishara ambayo haina gharama pia.

5. Zaidi ya hapo ni leseni za aina tofauti kulingana na aina ya bishara pamoja na VAT kama mzunguko wako Kwa Mwaka ni zaidi ya 40m

Mara nyingi inakuwa rahisi kama utamupa mwanasheria au yeyote Mwenye uzoefu afanye yote hayo other wise inasumbua sana kukamilisha Kwa muda mfupi unless huna haraka.

Kama unaswali niulize...



alfredmkohi@gmaildotcom
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…