Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kwa mujibu wa utafiti wa www.trustpilot.com wamefanya tafiti na kubaini kwamba kila mtu huwa anabeba chuki na kinyongo moyoni kwa vitu 7 kwa wakati mmoja.
Walifanya utafiti kwa kuchukua watu 12000 kutoka dunia nzima na walibaini kwamba 78% ya watu walibainika kuishi huku wakibeba chuki na kinyongo moyoni.
Kwa wastani mtu anaweza kubeba chuki na kinyongo moyoni kwa miaka 5 mfululizo, lakini 15% ya Washiriki walionekana kubeba chuki na kinyongo kwa miaka 11+ mfululizo.
KUSAMEHE MAKOSA NA MATUKIO HAINA MAANA YA
1.Kuondoa wajibu wa mhusika katika kosa au kitendo hicho
2.Kuunga mkono tabia au vitendo vya mhusika
3.Kuweka visingizio juu ya tabia ya mhusika kwa kitendo ambacho amefanya
4.Kusahau -Kufuta makosa ambayo mhusika amefanya katika kumbukumbu zako
5.Kurudisha mahusiano kama zamani.
Unaweza kusamehe makosa bila kufanya 1-5 hapo juu.
HATUA ZA KUSAMEHE MAKOSA
1.Kutambua kitu chenye kukuumiza
2.Kuhisi hisia zako (Ruhusu maumivu ya tukio husika yaje) (feel your feelings)
3.Jenga huruma kwako mwenyewe
tamka maneno ya faraja ambayo ungemwambia rafiki yako ûnampenda sana kama angekuwa anapitia hali kama ya kwako (Ukiwa na tatizo la kujichukia, kujilaumu,kujikosoa (harsh inner critic) unaweza kujisema vibaya sana lakini inakuwa na maneno mazuri kwa Watu wengine wakija kuomba ushauri kwako.
4.Badili tabia yako kwa tukio hilo
kama ulikuwa mpole kupitiliza, mvumilivu sana, mnyenyekevu,unapenda haki,unasaidia sana watu,unajitoa mhanga kwa watu wengine lakini jamii imeona kama UDHAIFU wako kisha umeibiwa, kudhulumiwa, kutapeliwa, kupokonywa mali, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kudhalilishwa hadharani, kufanywa kichekesho huo unakuwa wakati wa kujifunza kuwa mkali pale ambapo utovu wa nidhamu unapojitokeza,unaacha kusaidia watu wasiokuwa na faida kwako,unapiga marufuku utani wenye maudhi,unakata mazoea na watu ambao wanakuja kwako wakiwa na matatizo tu lakini wakiwa na furaha wanajitenga ili kuepuka kutumiwa kama tambara la deki.
5.Kubali kwamba mtu ambaye amefanya makosa huenda asije kuomba msamaha
ondoa dhana kwamba mtu ambaye amekusaliti,kukuibia, kukudhulumu,kukuzushia uongo,kukufukuzisha kazi,anatakiwa kuishi maisha ya dhiki sana halafu wewe upate mafanikio makubwa sana kisha aje kuomba msamaha au MSAADA wako kisha umjibu vibaya kama kisasi.
Hizo hadithi zipo kwbeye movies na tamthilia tu kwenye maisha halisi unaweza kuibiwa, kudhulumiwa, kutapeliwa, kupokonywa mali, kutukanwa, kujibiwa vibaya, kufukuzwa nyumbani usiku wa manane, kufukuzwa kazi, kufukuzwa nyumba ya kupanga,kufelishwa masomo lakini haoni hata siku moja mtu ambaye alikufanyia ubaya anapitia kipindi kigumu sana maishani mwake mpaka anakufa lakini maisha yako yatakuwa majanga tu kila siku..