Kusamehe ni njia bora ya kufungua milango yako ya baraka na kuondosha huzuni

Kusamehe ni njia bora ya kufungua milango yako ya baraka na kuondosha huzuni

third eye chakra

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2023
Posts
713
Reaction score
1,745
KUACHILIA/KUSAMEHE.

Ni pale unapokuwa huru ndani mwako,

Jambo hili linatupoteza wengi sana ,na mwishowe tunarudi kuwalaumu wachawi Kwamba ndio wanaotukwamisha mambo yetu kumbe hiyo ni sumu uliyokaa nayo ndani mwako ndio tatizo la mafanikio yako.

Kuna mtu unakuta ametunza kinyongo, ametunza Hasira, ametunza roho mbaya ,ametunza negativity za Kila aina na watu/vitu muda mrefu, hiyo ni sumu ambayo inakudhuru na kukurudisha nyuma mambo yako mengi, ikiwemo kutokuusikia ulimwengu jinsi unavyozungumza nawe, maana umejaa sumu ndani mwako.

Sasa basi jawabu ni kuachilia/KUSAMEHE na kuwa tupu ndani mwako. Ndipo UTAONA mambo mapya yanaanza kumea na kukua ndani mwako.

Hata kama mtu alikufanyia jambo baya Namna gani wewe jitahidi uliachilie/samehe .

KUSAMEHE ni dawa katika mambo yako yaliyokwama.

FB_IMG_17075594905176748.jpg
 
Wengi huona kusamehe humsaidia wanaye msamehe kumbe kiuhalisia inakusaidia zaidi wewe unaesamehe.Ndo maana ili uishi kwa amani na furaha muda wote samehe bila kuombwa msamaha.

Hata Muumba alisema katika

Isaya 43:25
Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.

Usiposamehe unakuwa umewabeba ambao hujawasamehe ndani yako bila kujua.
 
Upo sahihi ktk ulimwengu au universe msamaha huwa upo katika eneo linaloitwa detachment -kuachilia

Detachment ni kuliachilia jambo na kuruhusu jambo zuri lije au litokee.
 
Back
Top Bottom