1. Luka 17:3 āJilindeni, kama ndugu yako akikosa mwonye akitubu msameheā
Neno hili linaeleza habari za kugawana gharama, kwanza kama ndugu akikosa mwonye, pili akitubu msamehe. Upo uwezekano wa mtu huyo kukataa kutubu Je? Asipo kubali maonyo unafanya nini hapo. Usisubiri kuombwa msamaha ndo usamehe.
2. Warumi 5:8 āBali Mungu aonesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwakuwa kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambiā
Hii ni hatua kubwa ya msamaha ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo, kristo alikufa kwa ajili yetu tukiwa tungali wenye dhambi, alitangaza msamaha kwetu tungali watendaji wa mambo yaleyale ambayo ni chukizo kwake
Usisubili kuombwa msamaha, eti hajaomba msamaha nimeshindwa kumsamehe, alitakiwa kuombe msamaha ndo nimsamehe, kama unasubiri kuombwa msamaha ujue kuuona ufamle wa mbinguni kwako itakuwa ngumu
Lazima ukubali kubeba gharama zako na za yule unaye msamehe, kumuonya aliye kokosea ni kutaka kugawana gharama ambazo ulitakiwa kuzibeba wewe mwenyewe. Ukijivika ujasili utaweza kusamehe
Msamaha ni tiba ya nafsi, hurejesha kila kilicho potea, huleta upatanisho, huondoa hukumu, hurejesha mahusiano yaliyo potea
Zab 103 2-5 Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akutia taji ya fadhiri na rehema, aushibisha mema uee wako, ujana wako aurejesha kama tai.
Aliye kuumiza hawezi kukuondolea maumivu wala uliye muumiza huwezi kumwondolea maumivu, bali kristo mwenyewe ndani yetu ndiye awezaye kutuondolea maumivu, majeraha na machungu iwapo tu utampa nafasi.
Tendo alilolifanya Yesu lilikuwa la kijasiri, hata wewe unaweza kuwa jasiri kama Yesu kwakuwa hupo ndani yako, mruhusu akusaidie kufanya maamuzi magumu.
āNayaweza mabo yote katika yeye anitiaye nguvuā Nguvu ya kusamehe inattegemea maamuzi yako, Vile unavyo amua kusamehe ndinyo Mungu anavyo kutia nguvu za kusamehe
Unacho hitaji ni kusamehe na kusahau bila kujali kafanya nini na ni nani na kwanini ili uishi maisha furaha, kusamehe ni uwezo wa kukubali ukweli wa mambo.
Kusahau ni kukubali, huwezi kusahau kile mtu alichokufanyia, lakini yote unahitaji tu kufanya ni kukubali ukweli kwamba uliopita umepita na kuondoa chuki hizo moyoni mwako.
Huna haja ya kusubiri au kusikia mtu anakuja kwako kuomba msamaha ili umsamehe.
Haiwezi kamwe kuja. Hebu msamaha uwe maisha yako āTabia yakoā ambayo haitategemea tabia ya mtu mwingine, bali kwa moyo wako wa ukarimu.
Ebr 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna mtu atakaye muona Mungu asipokuwa nao. Kila mwenye matarajio ya kwenda mbinguni ni lazima roho ya msamaha iwe maisha yake, Utaishi kwa amani, kwa furaha, hutakuwa nauchungu kamwe.