SoC03 Kusanikisha Mfumo wa Rufaa za katika Hospitali za Kanda

SoC03 Kusanikisha Mfumo wa Rufaa za katika Hospitali za Kanda

Stories of Change - 2023 Competition

Alfris

Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
6
Reaction score
9
NAMNA ILIVYO SASA
Mfumo wetu wa Rufaa katika Hospitali za Tanzania, unategemea tu Barua ya Daktari mwenye hadhi ya kuandika Rufaa, na akishaandika, humkabidhi mgonjwa kwenda Hospitali aliyoelekezwa.

CHANGAMOTO
Siyo rahisi sana kuwa na hakika ya kushughulikiwa Rufaa husika. Pengine, Daktari ili atoe rufaa anaweza naye kudai rushwa. (Binafsi ilishanipata). Kuna ile kuambiwa "hebu angalia namna, nikuunganishe na Bingwa mmoja nina namba zake".

SULUHISHO
Hospitali za Kanda na hata za Mikoa na wilaya kama itafaa, ziwe na mfumo wa ki mawasiliano wa Kitaifa (KanzaData), ili, Daktari mara tu anapopelekewa mgonjwa na kuanza kumhudumia, mfumo unasoma ni nani anamhudumia nani, na huduma imekamilika ama bado. Kama ikiwepo Rufaa, Daktari mwenye hadhi afanye Rufaa kwa Mtandao, taarifa ziende hadi kwa Daktari na hospitali husika, na atakapofakinikiwa kumtibu mgonjwa, Rufaa irudi Hospitali ya awali.

INAWEZEKANAJE?
1. Itawezekana, endapo Madaktari wote watasajiliwa, watatambulika na mfumo wa kitaifa, wata
2. Itawezekana endapo huo mfumo utabeba taarifa zote za mgonjwa na kufuatilia endapo ameshughulikia rufaa yake, na kumkumbusha tarehe ya rufaa.

3. Itawezekana, endapo pia vituo vya afya na zahanati zitakuwa na mfumo utakaoshughulika na magonjwa ya kawaida, na kuacha rufaa ziende ngazi za kanda, badala ya hospitali za kanda kuhangaika na magonjwa mdogomadogo

4. Itawezekana, endapo hospitali za ubobezi zitaongezwa idadi.

5. Kwa vile uendeshaji ni wa Ki Digitali, mgonjwa hana haja kubeba File, ama kuogopa eti limepote, ama namba ya hospitali. Inatosha tu kujitambulisha na kupata taarifa zako.
Pia, badala ya kupanga foleni kujisajili, mfumo wa kutoa namba uwe wa ki digitali. Mtu aingie kuhudumiwa endapo Screen imeonesha namba yale.

NB: Mfumo utoe kipaumbele kwa wazee na watoto.


FAIDA
1. Ni rahisi kumfuatilia mgonjwa aliyepewa Rufaa na kuacha kwenda Hospitali, na kujua sababu za kutofuata Rufaa yake.
2. Ni rahisi kumuwajibisha Daktari endapo mgonjwa atapata madhara ya uzembe utokanao na Tabibu.
3. Itapunguza msongamano wa wagonjwa wasio na rufaa na wenye rufaa kwenye hospitali za kanda,.
4. Utaokoa maisha na kuepusha vifo visababishwavyo na upotevu wa muda
 
Upvote 1
Back
Top Bottom