Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Hayati Magufuli aliipiga marufuku biashara ya jongoo wa baharini ambayo kwa kiasi kikubwa inafanywa na raia wa China. Kwa Wachina jongoo bahari ni chakula murua (delicacy), na pia ana matumizi mbali mbali ya madawa. Utafaiti wa hivi karibuni unaonesha jongoo bahari ni tiba ya kansa hasa katika hatua za mwanzo.
Nimefika Kenya na kustushwa kuwa biashara hii inafanywa kwa ari kubwa na raia wa Kichina wakileta shehena kwa shehena kutoka Tanzania. Mchina niliyezungumza naye alidai kuwa jongoo bahari sasa ni adimu kupatikana katika mwambao wa bahari ya Hindi upande wa Kenya (labda wamewamaliza), na kwamba hivi sasa laziima uende bahari ya kina kirefu (deep sea) ndiyo uwapate, tena ukibahatika! Akaongeza kuwa Tanzania sasa ndiyo shamba lao kuu! Nilipomwuliza kwani China hakuna jongoo bahari? Alistuka na kurudi nyuma akasema, China ukigusa kiumbe chochote, kifungo chake watakusahau! Hata ndege, isipokuwa tu wale wa kufugwa.
Hapo kwa mara nyingine nikaona jinsi gani Waafrika hawafikirii mustakbali wa watoto wao. Nikaungaisha na jinsi nilivyosikitishwa kuona Twiga, Swara, Dikdik na chui, katika mbuga mpya iliyotengenezwa huko UAE , Emara ya Sharja. Huwezi katu kuona Panda, Koala, Kiwi, Kangaroo. Mahali pegine popote duniani isipokuwa China, New Zealand, Australia (nchi za asili yao) lakini vyetu vipo kila mahali duniani. Kwa mara nyingine upumbavu wa mtu mweusi wa kuuza kila kilicho chake bila kujali, kama walivyouza mababu zetu wana wao kwa shanga, ni ule ule. Hatujaendelea kamwe kiakili! Unashangaa huu ujinga na tamaa ya mtu mweusi vitaisha lini?
Siku moja tutaamka tukute vitu vyetu vyote, maji, mapori, wanyama, ardhi, havipo, tumebakiwa na hela tuzile! Kwa Tanzania, huyo aliyeuza yumkini ni rais wa nchi hasa! Tena atajiona mjanja saaaana kwa kufanya hivyo!
Haidhuru utafiti wa jongoo bahari bado unaendelea, ila mambo muhimu fulani yanajulikana. Kwamba jongoo bahari anasaidia kula fungi hatarishi kwa maisha ya samaki, pia jongoo bahari 'Nudibranchs' kwa kitaalamu anaweza kuwa dawa ya kuzuia au kuponya kansa katika hatua za mwanzo kutokana na kemikali kali anazozila. Jee, mnyama kama huyu tuko tayari tumpoteze?
Msemeni vyovyote Magufuli lakini 'passion' yake kwa kukinga mazingira hakuwa nayo rais yeyote zaidi ya Nyerere. Aliona mbali sana. Labda elimu yake ya sayansi chemistry ilimsaidia kutambua umuhimuwa vitu hivi. Katika safu ya viongozi wetu wa sasa, bado namtafuta kiongozi mwenye 'passion' ya kitu chochote zaidi ya mpira wa miguu!