SoC03 Kushinda vita ya elimu

SoC03 Kushinda vita ya elimu

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Jun 25, 2023
Posts
45
Reaction score
32
NENO LA MUNGU LINASEMA: "Mkamate sana ELIMU, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni UZIMA wako." (Mithali 4:13)

Swali ni je! Unadhani Elimu uliyo nayo sasa ndiyo hii tuliyoambiwa tuikamate sana tusiiache iende zake na tuishike maana ni UZIMA wetu?

SIFA ZA ELIMU YA MUNGU NA TOFAUTI KATI YA ELIMU YA MUNGU NA ELIMU ISIYO YA MUNGU

ELIMU YA MUNGU Hufundisha kujiajiri wakati elimu isiyo MUNGU hufundisha kuajiriwa. Hapo mwanzo MUNGU Hakuajiriwa wala Hakuambiwa na mtu yeyote Aiumbe dunia, bali YEYE MWENYEWE Aliamua Kujiajiri; Kufanya KAZI HII NJEMA YA KUUMBA MBINGU na nchi (Mwanzo 1:1)

ELIMU YA MUNGU Imejikita kwenye MAFUNZO KWA VITENDO VYA HALI YA JUU vyenye kumpelekea mjifunzaji KUELEWA VIZURI MNO anachojifunza na kuyafanya mawazo yake yawe yaani yatimie ulimwenguni kwa vitendo (Mwanzo 1:1-3) (Yohana Mtakatifu 7:15-16) wakati Elimu isiyo ya MUNGU imejikita kwenye maneno mengi, kukariri na vitendo vichache au vitendo hewa, hata kupelekea mwenye Elimu hii kuiishi Elimu yake kinadharia zaidi badala ya kuiishi Elimu yake kwa vitendo.

ELIMU YA MUNGU Hufuata NENO LA MUNGU Linavyosema na Hubeba UBUNIFU, HEKIMA, MAFUNZO, MAARIFA, UJUZI NA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA ya hali ya juu ambayo humpelekea mwenye kuipata ELIMU HII abuni mambo mapya na makubwa ambayo hayajawahi kutokea katika ulimwengu huu ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili ulimwengu kama vile MUNGU Alivyotumia UBUNIFU, HEKIMA, MAARIFA, UJUZI NA TEKNOLOJIA YA HALI YA JUU KUUMBA ulimwengu mpya ambao hapo mwanzo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto za giza, utupu na ukiwa (Mwanzo 1:1-2) (Kutoka 31:1-6) (Kutoka 35:30-35); wakati elimu isiyo ya MUNGU inakusudia kupingana na ELIMU YA MUNGU ikiwemo UBUNIFU NA TEKNOLOJIA YA HALI YA JUU, badala yake hufuata na hu 'promote' mawazo na falsafa za watu; walio hai, waliolala mauti na wengineo. Hii ni Elimu ya "according to Mawe Maembe..." "According to Miti Mia..." "(Kiredio Kisabufa 2003, ...) na Kadhalika, pasipo kujua kuwa wakati Mawe Maembe, Miti Mia na Kiredio Kisabufa wanayasema hayo yanayoingizwa kwenye fikra za watu walikuwa kwenye hali gani, mahali gani au wakati gani.

ELIMU YA MUNGU imejikita kwenye KUAJIRI na KUWA CHANZO CHA AJIRA kwa wanadamu kama MUNGU Alivyopanda BUSTANI na kisha Kumwajiri Adamu ailime na kuitunza (Mwanzo 2:8, 15-17); wakati elimu isiyo ya MUNGU imejikita kwenye kumnyang'anya au kumpokonya mwanadamu hata ajira yake aliyo nayo kwa kusababisha mwanadamu kumkosea MUNGU ili afukuzwe kazi yake kama Adamu na Hawa walivyofukuzwa bustanini (Mwanzo 4:24). Hii ni kwa sababu elimu isiyo ya MUNGU husababisha wimbi kubwa la ufisadi, ulaji rushwa, utapeli, uongo, utumwa, mabaya ya kila namna yasababishwayo na kupenda fedha (1 Timotheo 6:10) na katika ulimwengu tuliopo hakuna taasisi inayoweza kuvumilia kufanya kazi na mfanyakazi mwenye tabia hizi.

ELIMU YA MUNGU Imebeba BARAKA NA UZIMA kwa ajili ya wanadamu duniani kote (Mithali 4:13) wakati elimu isiyo ya MUNGU imebeba laana na mauti kwa ajili ya wanadamu duniani kote. Hii ndiyo sababu pamoja na kuongezeka kwa idadi kubwa ya wasomi duniani kote kila siku asubuhi, mchana na jioni, ndivyo kiwango cha magonjwa, umaskini, uasi, vita, njaa, rushwa, ufisadi, huongezeka siku hadi siku Afrika.

ELIMU YA MUNGU 'title' yake pekee kwa aliye nayo ni 'FUNDI' kwa kuwa ni ELIMU ILIYOBEBA MAFUNZO YA UFUNDI. Title hii ni HURU hivyo ni ruksa kutumika na Mwanadamu yeyote bila kunyooshewa vidole wala kusimangwa hata kama mwanadamu huyu hana ELIMU hii wakati elimu isiyo ya MUNGU ina 'title' ya ubinafsi kwa aliye nayo inayosababisha uchoyo, utumwa na masimango kwa wanadamu wengine ambao hawakupata Elimu hii pale wanapotaka kutumia title hizi. (Mithali 8:31-32) (Marko 6:3)

ELIMU YA MUNGU ni nira laini na mzigo mwepesi, (Mathayo 11:28-30) haichoshi wala haimuelemei msomi wa ELIMU HII bali humfanya aipende kutoka moyoni na kuitumia katika maisha yake yote baada ya kupata ELIMU HII wakati elimu isiyo ya MUNGU ni nira ngumu ambayo hugeuka kuwa kitanzi kwa msomi wa elimu hii, na ni mzigo mzito wenye kumwelemea msomi wa elimu hii hata kumfanya aichukie elimu lakini hana namna, kwa kuwa asiposoma jamii itamwona kilaza (Isaya 10:27). Lakini pia ni elimu ambayo msomi haioni thamani yake, yaani anaweza kusoma elimu kuhusu rasilimali watu lakini akishamaliza kama hatopata ajira ya rasilimali watu basi anaachana na rasilimali watu na kufanya kazi nyingine mfano kilimo, ufugaji, ujasiriamali, biashara, na kadhalika.

ELIMU YA MUNGU
hukuza kipaji yaani Talanta ya msomi wa ELIMU HII (Mathayo Mtakatifu 25:28), wakati elimu isiyo ya MUNGU hukusudia kuangamiza kipaji yaani Talanta ya msomi wa elimu hii na kumwacha na mawazo ya kina Mawe Maembe pekee.

ELIMU YA MUNGU Gharama zake za malipo ya ada na kadhalika ni za kiasi, zinazomwezesha msomi wa ELIMU HII kusoma na kumaliza masomo yake bila usumbufu wowote wakati elimu isiyo ya MUNGU Gharama zake za malipo ni kubwa sana hata kufikia msomi wa elimu hii kushindwa kumaliza masomo yake au kushindwa kujiunga na ngazi zinazofuata za elimu anayotaka kusoma kwa sababu mbalimbali za kiuchumi.

NENO LA MUNGU LINASEMA: "Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika MUNGU hata kuangusha ngome; tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya ELIMU YA MUNGU; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii KRISTO;" (2 Wakorintho 10:3-5)

Kumbe! Taifa la Tanzania na Afrika kwa ujumla tunatakiwa tubadili MFUMO WETU WA ELIMU kuwa ELIMU YA UFUNDI kwani ndiyo ELIMU YA MUNGU Aliyokusudia tuipate lakini si Elimu hii ya Ufundi ya VETA iliyopo nchini Tanzania, bali ni ile Elimu ya Ufundi yenye HADHI NA MATUMIZI YA HALI YA JUU YA UBUNIFU NA TEKNOLOJIA, iliyo kwenye Mataifa Makubwa duniani, kwani wao pia wanafahamu kuwa Elimu hii ndiyo Dhahabu na wanaijua nguvu iliyo katika Elimu hii ndiyo maana huminya Scholarships za Elimu ya Ufundi kwenye mataifa yao zisitolewe ovyo Afrika ili waafrika wakose UBUNIFU wa kufanya mambo makubwa na hata ikitokea miradi mikubwa kwetu bado tuendelee kuwaita wao waje kuwa Wahandisi Wakuu wa miradi hiyo licha ya kwamba wasomi wanaongezeka siku hadi siku barani Afrika. Tafsiri yake ni kuwa elimu tuliyo nayo sasa Afrika ni elimu iliyochakachuliwa na mawazo na falsafa za watu ili bara hili la Afrika liendelee kuwa BARA LA WATUMWA.

SIMAMA TANZANIA! SIMAMA AFRIKA! UHURU KUTOKA KWA BWANA UMETUJILIA💪
 
Upvote 2
Back
Top Bottom