Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,440
- 8,149
Jamaa walilipa advansi tu, mzigo ushakamilika kule Mumbai kwa ndugu zake MO ingawa wafuasi washajazwa kwamba zinatengenezwa ulaya, Sasa wahindi wanataka pesa yao ili watoe mzigo na Barbra pesa yote alishatafuna, Vunja bei alitaka atangenezee jezi kwa jamaa zake wa China, Barbra akafosi kuwa Kuna mtu wake kule Mumbai ndo atatengezeza jezi, baada ya mvutano wa muda mrefu Vunja bei akaona isiwe tabu akamueleza Barbra bajeti aliyopanga kutengenezea jezi kule China, Barbra akataka apewe hizo pesa ili mchakato ufanyike India, basi Vunja bei akatoa mzigo kwa CEO kwa maandishi. Utata ni kwamba Hadi Sasa kimya, hakuna Cha jezi wala soksi, na Fred keshawaeleza viongozi wa simba hali halisi, kufuatilia ndo ikaonekana mzigo uko tayari ila shida ni malipo hayajakamilika, Klabuni hakuna pesa ili waokoe jahazi Sasa wanategemea huruma ya mdosi MO awadhamini kwa wadosi wenzake ili waachie mzigo.