Kushindwa kumalizia Pesa ndio kikwazo kwa Simba kushindwa kupata jezi hadi Sasa

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
8,440
Reaction score
8,149
Jamaa walilipa advansi tu, mzigo ushakamilika kule Mumbai kwa ndugu zake MO ingawa wafuasi washajazwa kwamba zinatengenezwa ulaya, Sasa wahindi wanataka pesa yao ili watoe mzigo na Barbra pesa yote alishatafuna, Vunja bei alitaka atangenezee jezi kwa jamaa zake wa China, Barbra akafosi kuwa Kuna mtu wake kule Mumbai ndo atatengezeza jezi, baada ya mvutano wa muda mrefu Vunja bei akaona isiwe tabu akamueleza Barbra bajeti aliyopanga kutengenezea jezi kule China, Barbra akataka apewe hizo pesa ili mchakato ufanyike India, basi Vunja bei akatoa mzigo kwa CEO kwa maandishi. Utata ni kwamba Hadi Sasa kimya, hakuna Cha jezi wala soksi, na Fred keshawaeleza viongozi wa simba hali halisi, kufuatilia ndo ikaonekana mzigo uko tayari ila shida ni malipo hayajakamilika, Klabuni hakuna pesa ili waokoe jahazi Sasa wanategemea huruma ya mdosi MO awadhamini kwa wadosi wenzake ili waachie mzigo.
 
Kwani Simba ndiyo wanaagiza jezi wewe ndezi? Mnakimbilia kuanzisha thread za kizushi bila kuwa na facts. Nyie kweli ni kima kama alivyosema Luc Eymael

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kama vipi tuanadamne tu kwenda kwa mwekezaji. Haiwezekani muda unazidi kuyoyoma, halafu jezi hatuzioni!!
 
Yanga wanafuatilia zaidi habari za Simba kuliko Simba kwa Yanga.
 
Jezi zinatoka ulaya wewe unaleta habari ya India, utopolo ni mzigo wa matope tunahangaika nao kuubeba kila siku.
 
Kama vipi tuanadamne tu kwenda kwa mwekezaji. Haiwezekani muda unazidi kuyoyoma, halafu jezi hatuzioni!!
Muandame kwenye zile jezi zenu kuna mitaa ya ya jiji la daslam
Au wewe hujanunua ile jezi?
 
Tatizo utopolo mnazisubiri jezi ili mlinganishe na historical sites zenu
 
Tunaoumia ni sisi mashabiki halafu wao wanachukulia vitu easy tu! Sisi kama mashabiki na wanachama hai tuna haki ya kuhoji, hatutaki siasa na porojo

Na mimi binafsi naona kuna uzembe umetokea hawataki kuweka wazi (wataaibika) na ndio maana wanajificha kwenye kichaka cha ''SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WETU'' na Mdhamini.... Kipindi chote hicho walikuwa hawajui kuwa mkataba na Sportpesa unaisha msimu huu, juzi hapa wakapata aibu ile ya kubandua logo ya mdhamini wa zamani wakaweka mdhamini mpya juu kwa juu (hii tunaita kukosa weledi)

Tukubali tu pale kuna kiongozi fulani hajawajibika ipasavyo au anatufanyia hujuma au kuna mgongano wa kimaslahi na kusababisha UZEMBE na sintofahamu hii kwa mashabiki hadi leo...(YAPASWA ALAUMIWE naawajibishwe kwa onyo)

Wenzetu majirani wao wamewahi na kesho kwenye JAMBO LAO wanakinukisha sisi tunabaki mtaani macho kodo tunaringishiwa na mtani.

Sisi kama mashabiki lialia wa Lunyasi mnyama tunaomba uzembe huu usijirudie...

Kutoka tawi la Mpira na Maendeleo - Fire Upanga Magharibi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…