KUSHINDWA KUOGELEA Kwa mbegu za Kiume

KUSHINDWA KUOGELEA Kwa mbegu za Kiume

ERIC JOSEPH

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2011
Posts
567
Reaction score
55
Mwezi uliopita tulienda hospitali ya mimi na mke wng kutokana na tatizo la kutopata mtoto mana sasa takilibani miaka 3.baada ya vipimo ndipo yeye alipo kundulika kuwa anamatatizo ya milija ya uzazi na amepangiwa upasuaji mwezi upasuaji mwezi ujao.upande wangu nikagundulika kuwa mbegu zangu za kiume hazina uwezo wa kusafili hapo doctar aliniambia kuna dawa japo hakuniambia ni dawa ipi.naomba ushauli wenu mana naumia sana kwa kutokuwa na mtoto japo moja.samahan kwa maneno mengi.naomba ushauli wenu
 
Daktari gani anayetoa matibabu nusu? Muungwana Eric rudi mwone tena huyo mtaalam kwa sabau kiujumla kama maelezo yako ni ya kweli tatizo lako lina gusia swala la zima fertility quality kwa upande wako hii ikiwa ni pamoja na sperm quantity and sperm quality.

Ushauri wangu onana na wataalamu haswa wa maswala haya.
 
Nashukulu ni kweli sasa je hapo nikaombe dawa au kunaushauli wa ziadaNDG yng

kabla hujaomba dawa nadhani ni vizuri kujua nini hasa tatizo lako kwa maana ya wewe nawe kufanyiwa uchunguzi na vipimo kama mwenzako. dawa zije baada ya kubaini pasipo shaka kuwa nini hasa tatizo lako.
 
Asante

Kama alivyosema MJ, ni vizuri ukapata habari zaidi ni nini hasa tatizo kuliko kuambiwa tu juujuu. Ikiwezekana kabisa nenda kwa mtaalamu mwingine.
 
Ushauri: Muombe daktari akutibu kwanza wewe, then mjaribu kutafuta mtoto. Msipopata ndio mkeo afanyiwe upasuaji. Vinginevyo mnaweza kosa mwana na maji ya moto kwani upasuaji wa mirija ya kike ya uzazi sio tiba ya kuaminika sana au utatuzi muafaka wa tatizo la kukosa mtoto.
 
Asanteni kwa ushauri wenu nahitaji kusonga mbele mmeniongezea wazo jingine
 
Back
Top Bottom