Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Imeelezwa kuwa athari za corona nchini India ikiwemo idadi ya maambukizi na vifo imeshuka kwa kiwango cha juu bila kupatiwa maelezo ya kitaalamu.
Awali ugonjwa huu ulipoanza hapo mwaka jana ilikisiwa kuwa taifa hilo la pili kwa idadi ya watu duniani lingeathirika zaidi.Kuna kipindi maambukizi kwa waliopimwa ilifika watu laki moja kwa siku lakini kwa sasa ni watu elfu 10 tu na vifu vimepungua sana miongoni mwa walioambukizika.
Baadhi ya wataalamu wametaja hali hiyo huenda ni mafanikio ya uvaaji barakoa ambao umefanywa kuwa ni lazima kwenye miji mingi ya nchi hiyo.Hata hivyo hoja hiyo imekinzana na ukweli kuwa utekelezaji wake katika baadhi ya miji ni wenye kulegalega wakati kushuka kwa maambukizi hayo kuko karibu sawa kwenye miji yote.
Hoja nyengine imesema kuwa kushuka kwa athari za maradhi hayo ni kutokana na kuwa idadi kubwa ya wananchi wa India hasa vijijini wanafanya kazi zao maeneo ya wazi na wanalala majumba ya wazi.
Maelezo mengine ya baadhi ya watafiti ni kuwa kwa vile watu wengi tayari wamepata maradhi ya corona na kupona basi kumepatikana kinga za vikundi dhidi ya maambukizi mapya.
Wengine wamesema hali hiyo inatokana na kuwa wananchi wa nchi hiyo tangu wanapokuwa wadogo huwa wanaugua maradhi mengi ya maambukizi kama vile kifua kikuu na hivyo miili yao huwa imejenga kinga ya ndani kwa ndani ambapo wadudu wa corona wanapata shida kupenya kikamilifu kwenye mifumo yao.
Kubwa zaidi kuhusu hali hii ya janga la corona nchini humo imetokea hata kabla ya kuanza kutumika chanjo mwezi uliopita ambazo mpaka muda huu zimewafikia watu wachache sana kati ya idadi ya watu wote wa nchi hiyo wanaotakiwa kupewa chanjo.
Ikumbukwe kuwa taifa la India ndilo linaloongoza duniani kwa matumizi ya vyakula asilia na viungo vikali katika vyakula vyao.
Chanzo: India's dramatic fall in virus cases leaves experts stumped