Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Kwanza niwapongeze EWURA kwa ‘at least’ kuonesha kwamba wanamjali mwananchi wa chini. Bei ya mafuta (petrol) imeshuka karibu kwa asilimia 28% kutoka wastani wa Tzs 2,100 iliyokuwepo kuanzia mwanzo wa mwaka huu (Pre-Corona Crisis) mpaka bei ya sasa ya Tzs 1,500 kwa lita.
Katika kipindi hicho hicho mafuta katika soko la dunia yaliporomoka karibu kwa asilimia 71%, kulikosababishwa na sababu kuu mbili;
Technically, hizo ndo sababu halisi za kuanguka kwa bei ya mafuta duniani, sio kwa sababu ya serikali ya awamu ya tano, sio kwa sababu ya CCM, sio kwa sababu ya Magufuli, sababu haswa ni ‘MSUKUMO WA NGUVU YA SOKO – Demand and Supply’ ambao ni msingi wa uchumi wa kibepari.
So kwa upande mwingine nawapongeza EWURA kusimamia nguvu ya soko na mafuta kushuka kama ilivotokea duniani, ila bado walistahili kufanya zaidi, kwa hali ya soko la mafuta ilivokuwa tungeweza kabisa kustahili kuwa na punguzo la hadi asilimia karibia na 50%.
Sio furaha ya kudumu
Ukiangalia hii chart inajieleza yenyewe, mafuta yalifika karibu $16.17 per barrel (Mwezi April), halafu huku kwetu tumepata punguzo letu baada ya miezi miwili.
Tangu mwezi April mpaka sasa kwenye soko la dunia, mafuta yamekuwa yakiongezeka kutoka bei ya chini kabisa ya $16.17 per barrel mpaka sasa yanacheza kwenye $40.00 kwa barrel moja.
Hii inakupa tafsiri gani? Ina maana ya kwamba tegemea kabisa baada ya mwezi mmoja au miwili, bei ya mafuta hapa nchini inaweza kabisa kurudi kule ilipotoka (Tzs 2,100 kwa lita).
Na kile kilichotokea kwenye sukari kinaenda kutokea tena kuanzia mwezi mmoja unaokuja, makampuni mengi ya mafuta yataanza kuficha mafuta kwa sababu wanajua bei itaenda kupanda na tayar kuna hizo signals hata kwenye soko la dunia.

- Kuporomoka kwa mahitaji ya mafuta duniani kutokana na hatua za lockdown ili kupambana na covid-19 (Contraction in demand due to Covid-19); baada ya mlipuko wa Corona nchi nyingi duniani zili adopt lockdown ambayo technically ilizima shughuli nyingi za uzalishaji kwenye chumi nyingi duniani. Hii ilipelekea anguko la haraka la mahitaji na matumizi ya mafuta duniani. Na kiuchumi, demand inapoanguka kunakuwa pia na pressure ya bei kuanguka na ndicho kikubwa kilichotokea.
- Mataifa ya OPEC+ kushindwa kuafikiana kupunguza supply ya mafuta; baada ya anguko la demand (kwenye point namba moja) OPEC wangeweza kuzuia bei kuporomoka kama wangekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta (Supply cut). Lakini ilishindikana kufanyika hivo na matokeo yake, Russia na Saudi Arabia wakaingia kwenye vita vya kuzalisha mafuta. Ni sawa sawa uende pale Temeke, ukute siku hiyo nyanya zimekuja kwa wingi, hapo unategemea nini? Bei lazima itashuka, na ndo kilichotokea.