Habari Wakuu
Naomba msaada wa kujua sababu zipi zimepelekea bei ya ufuta kushuka.....kwa mfano mkoa wa Pwani hususani wilaya ya Rufiji wanunuzi ama walaguzi(waachuuzi ) walianza kununu ufuta kwa bei ya shilingi 1800 kwa kilo moja ya ufuta..... lakini tangu tarehe 10/6/2016 wamepunguza na kununua kwa bei ya shililgi 1600 kwa kilo.Je kuna nini uko katika soko la ufuta wanapopeleka hawa wanunuzi wachuuzi?