Kushuka kwa elimu shule za kata

galamtala

New Member
Joined
Dec 22, 2013
Posts
2
Reaction score
0
Kufanya vibaya kwa shule za sekondari za kata Tanzania unachangiwa na utaratibu mbovu na chuki binafsi kwa baadhi ya walimu wakuu.Wanawachukia sana walimu wa sayansi,hata kama mwalimu hana matatizo,naomba wadau wa elimu walivalie njuga hilo,ili kulinusuru Taifa.
 
Hii mara nyingi hutokea pale walimu hao wa sayansi wanapotanguliza maslahi mbele kutumikia tuition centers zao binafsi na kusahau madarasa yao,na mkuu kama bosi wao na akiwa responsible enough lazima awakazie
 
Duh, hili nilikuwa silijui;

Mwalim anaetumikia tuition centre zaidi kuliko shule huyo ni mzembe binafsi, maana kunawalim hawana hizo centre na watoto wanafeli, watoto kufeli masomo ya sayansi kwa hapa tz ni suala la saikolojia.

Pia masomo haya yanahitaji kujitolea kwa mwalim na mwanafunzi maana si mchezo,

Kitu kingine ni kwamba masomo haya yanahitaji constant learning la sivyo unasahau kila kitu, je ni wangapi wanapenda kujisomea?

Pia masomo haya yanahitaji resource nyingi tu hasa vitabu na bahati mbaya vitabu vya masomo ya sayansi vinauzwa bei ghari sana, je nani anaweza kununua? (mfano Abbot, Lambert, nelkon nk)

si hayo tu na sababu nyingine nyingi, mfano idadi ya hao walimu na mikondo anayotakiwa kufundisha per kidato (unakuta walimu wa somo moja wanaweza wakawa wawili form 1-4 na kila kidato kina mikondo zaidi ya miwili, je wataweza na hata kama wakiweza, je ni kwa mshahara upi?
Kumbuka siku hizi walimu tunasema "FUNDISHA KADRI UNAVYOLIPWA-(FUKU)"
 
Nimependa hii 'fundisha kadri unavyolipwa' yaani ( fuku) kwani ualimu sio wito tena ni kazi kama kazi nyingine mimi pia nikiwa kama mwl. Wa degree ntajitahidi niwe na tuition centres kibao kwani mshahara tunaolipwa ukilinganisha na fani nyingine ni aibu tupu sekta ya ualimu kwa hapa tanzania inaonekana haina mchango kwa maendeleo ya nchi hii kabisa ni vyema walimu wakajihusisha zaidi na mambo investment zao binafsi na tuachane na hao mbwa wanaowapuuza walimu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…