Ninapinga maamuzi ya kurudisha fimbo rasmi ingawa ukweli zilikuwa zikiendelea kama kawa!Sababu ni mbili tu za msingi.
1.Kutokana na matatizo ya serikali kupuuza madai ya walimu,walimu wengi wanaishi kwa stress na wakikabiliwa na matatizo lukuki ya kisaikolojia.Hivyo mtoto anaweza kufanya kosa hata dogo tu akapata kichapo cha mbwa mwizi!ama akaadhibiwa kwa makosa ya mtu mwingine.Mfano mie niliwahi kuadhibiwa vikali kwa kosa la kuchelewa shule mchana nikiwa nimetoka nyumbani ambako hata chakula sikuwa nimekula baada ya kukuta chakula hakijawa tayari,niliona nirudi tu shule,ndipo nilipokutana na kichapo kikali nikiwa nimeshika masikio!alitokea mwl mmoja akaingilia kati na baadae nikaja kujua kumbe yule mwl Mkuu aliyeniadhibu,alikuwa na ugomvi binafsi na baba mzazi ambaye eti alimchukulia demu wake!kichapo nikachezea mie!
2.Mtoto anaweza kuwa mtukutu kutokana na migogoro ya ndoa na ikamchanganya kisaikolojia.Watoto kama hawa ni wengi sana.Badala ya kuwasaidia,itakuwa kama kuwafanyia ukatili mara ya pili!most teachers are bitter kutokana na maisha wanayopitia!Nasikitika watu wanasoma sayansi ya jamii lakini wako kimya tu na hawapigii kelele maamuzi haya mabaya.Watoto wamefanyiwa ukatili mwingi ni nani mtetezi wao?Tafakari,kisha chukua hatua!
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums