Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Wiki ya jana tulijiuliza swali zima la ni kipi kinatakiwa hasa kwenye suala la kuosha vyombo baada ya kula na ikaonekana watu wengi wamekubaliana kuwa vyombo vinatakiwa kuoshwa kwa pamoja lakini kama mmoja anajitolea basi si vibaya na si jambo baya. Ilikuwa ni elimu tosha kwa watu wa majumbani na wenzi wao kujifunza umuhimu wa kuangalia na kutunza vyombo wanavyotumia. Shukrani.
Leo hata hivyo, mjadala wa leo unahusiana na jambo la kawaida sana lakini ambalo pia nimewahi likisababisha mgogoro wa aina yake. Vijana walikuwa wanajadiliana huku mmoja akionesha masikitiko yake kuwa mke wake kamnunia baada ya "kumshukuru" baada ya chakula. Kijana alisema "Nilimuambie mke wangu 'asante kwa chakula'" na yule mwanamke akaja juu. Kwamba, chakula ni haki yake, na ni yeye analeta vikapikwa hapo nyumbani kwanini ashukuru?
Mke wake akaja juu na kusema anayetakiwa kushukuriwa namna hiyo ni "mama ntilie" kwani wao huleta vitu vyote wao wenyewe na "kukuuzia" kwa hiyo kuwashukuru kwa chakula ni jambo muhimu sana kama unataka kuendelea kula kwa mama ntilie yule yule, lakini pia kuwa "mama ntilie" wao hawajali hata hiyo asante yako wao wanachotaka ni pochi tu. Kumbe mwanamke alikuwa offended kushukuliwa kwa "chakula" kwani hakuwa anauza na ni haki ya baba mwenye nyumba.
Kijana mwingine alipigwa na butwaa na kuanza kumcheka mwenzie huku akimshangaa:
"Yaani wewe unamshukuru mke wako kwa chakula" alihoji kwa kebehi.
"Sasa jamani ndivyo nilivyolelewa" alijibu kijana wa kwanza.
"Wenzio ndani ya nyumba zao hawashukuru kwa chakula ni mwiko" alisema jamaa kwa msisitizo.
"Really"? alihoji yule mwingine na kuongezea "sasa nifanyeje?"
"Unatakiwa kushukuru kwa mapishi!" alisema na kuweka kituo.
"mapishi!?" alihamaki
Ndipo akaendelea kumuelezea kwa kirefu kuwa vyakula vinaweza kutumia vitu vile vile karibu sehemu zote lakini ufundi wa mpishi ndio unatofautisha utamu wa chakula. Sasa usipomshukuru mke wako kwa mapishi yake mazuri maana yake chakula alichokupatia hakina tofauti na vyakula vingine. Jamaa akapewa elimu kuwa wapishi wote hutofautiana hata kama wanatumia jiko lile lile!
Ndio akaeleza ukiangalia sana kama mtu anapewa mapishi mazuri kwa 'mama ntilie' basi hata nyumbani atakula kwa kumridhisha 'mamii tu' lakini baadaye ataenda kupata bata wake wa kukaanga huko au samaki wa kukaanga! Na wakati mwingine mtu huufungia safari wali wa biriani maili nyingi kadhaa kwani mapishi yake huenda na mambo mengi.
Jamaa alielewa na alirudi nyumbani na kumuomba radhi mke wake kwa kumfanya kama mama Ntilie. Walipomaliza kula usiku ule jamaa alijilamba na vidole na kuanza kumwaga sifa za mapishi na utamu wa karibu kila kiungo. Mke wake alifurahi na uso uling'aa kama mbalamwezi na tabasamu kama aliyeona hazina ya dhahabu.
Jamaa alijua amemfurahisha mke kweli kwa kumshukuru kwa mapishi; kabla hajakaa sawa mamii akamuuliza "unataka desert?"