Kushusha Sukari Kienyeji

Kushusha Sukari Kienyeji

Ulipojaribu tiba lishe ya mchicha kudhibiti kisukari

  • Ndio ilishusha sukari

    Votes: 3 21.4%
  • Hapana sukari ilibaki vilevile

    Votes: 2 14.3%
  • Sukari ilizidi badala ya kupungua

    Votes: 0 0.0%
  • Sielewi

    Votes: 7 50.0%
  • Sikujaribu

    Votes: 2 14.3%

  • Total voters
    14

Mlenge

R I P
Joined
Oct 31, 2006
Posts
2,125
Reaction score
2,306
Kushusha Sukari Kienyeji

Pole kwa wote wanaosumbuliwa na sukari iliyozidi kwenye damu (kisukari).

Nimepata kusikia kwa watu fulani wakisimulia walivyofanikiwa kushusha sukari kwa haraka na kwa mafanikio. Kabla ya kueleza zaidi, tafadhali zingatia yafuatayo:

1. Mimi siyo daktari wa tiba za kisasa wala za kizamani za binadamu, hivyo usichukulie haya kama ushauri wa tiba.
2. Hakikisha unafikia mashine ya kujipima wingi wa sukari kwenye damu, kwani mbinu tajwa huweza kushusha sukari.
3. Endapo utaamua kujaribu mbinu hii, utafanya hivyo kwa hatari/hasara yako mwenyewe (at your own risk).
4. Ukipenda, leta mrejesho hadharani, endapo utatumia mbinu tajwa.

MBINU
1. Pima wingi wa sukari mwilini. Fanya yafuatayo, iwapo sukari ni kiwango kikubwa kuliko inavyotakiwa.
2.Chukua mchicha kiasi fulani (fungu moja hivi). Usafishe kwa maji safi.
3. Saga mchicha (tumia mashine - blender - au twanga mchicha kwenye kiuri).
4. Kunywa kimiminika kitokeacho, kikombe kimoja.
5. Jipime kiwango cha sukari mwilini.

Kama hii inasaidia kweli, basi kila la kheri.

Edit 1: Uzi umepokea posti za wanaodai wana tiba mbadala za kisukari. Sihusiki nao.
Edit 2: Matokeo zaidi yanaweza kupatikana kwa kula nyama, samaki na mboga za majani pekee kwa siku mbili au tatu kama nyongeza.
Edit 3: Piga kura hapo juu kushea uzoefu wako.
 
Mkuu unaujua vizuri ugonjwa wa kisukari kwa maana chanzo chake na aina zake? Watu hudanganywa kua kuna dawa ya kutibu kisukari lakini kiuhalisia hiyo dawa haipo

Wanaojiita matabibu wa huo ugonjwa hukimbilia kuchukua pesa ya mgonjwa in advance kisha baada ya hapo anapewa lundo la madawa ya kienyeji tena makali ambayo kwa hakika yanahatarisha afya ya figo na ini kwa mtumiaji.

Hayo yametukuta kwa Mzee wetu. Huwezi kupata tabibu hata mmoja ampe mgonjwa dawa kwanza aangalie kama itamsaidia ndio aanze kulipa pesa. Wote wanataka pesa mbele tena nyingi na baada ya matumizi kama haijasaidia (pengine inashusha sukari kwa kiasi fulani tu na sio kutibu kongosho) basi hutoa maelezo ya kisanii kuhusu kushindwa kwa dawa husika
 
B
Mzee bado mgonjwa?!
Yes, bado anaumwa japo anaendelea vizuri kwa kutumia vyakula na dawa za hospitali ambazo kwa hakika haziponyeshi kisukari bali zinasaidi tu kushusha kiwango cha sukari kwenye damu

Tumejitahidi sana kumtafutia tiba za asili lakini tatizo ni kwamba kila anayesema ana dawa anakuhakikishia kua hiyo ndio yenyewe, watu wengi wamepona na kwamba lazima muilipie, tena bei zao sio ndogo. Mwisho wa siku mnagundua kua nayo hiyo ni dawa ya kupunguza tu kiasi cha sukari kwenye damu na muda wowote akiacha masharti ya vyakula au akiacha dawa za hospitali inapanda tena!
 
Yes, bado anaumwa japo anaendelea vizuri kwa kutumia vyakula na dawa za hospitali ambazo kwa hakika haziponyeshi kisukari bali zinasaidi tu kushusha kiwango cha sukari kwenye damu....

Poleni. Mmejaribu hii ya juisi ya mchicha mbichi?
 
Tutajaribu hiyo pia mkuu asante sana, ingawa nayo itakua ni yakushusha sukari kwa muda huku mgonjwa akiendelea kufuata masharti yote ya mtu mwenye kisukari. Unajua tatizo ni kongosho linakua limeathirika na ni kama ulemavu hivi

Jaribuni kiongozi.

Pana mtu alijaribu hii ya mchicha, sukari ikashusha sana, mpaka ikamlazimu kuanza kuipandisha. Ndio maana ni muhimu kuwa na vipimo. Ni kweli ni muhimu pia kuendelea kufuata masharti ya mtu mwenye kisukari. Usikate tamaa, mwili wa binadamu ni huwa unajirekebisha wenyewe. Unaweza kukuta kwa kuendelea kufuata masharti wakati sukari iko kawaida kongosho likarudi hali yake ya kawaida.

Na hapo kwenye kufuata masharti, kitabu cha Dk. Boaz Mkumbo cha Sayansi ya Mapishi kimeongelewa vema na watu kwamba kimekuwa cha msaada kufafanua kuhusu lishe stahiki. Unaweza kukisoma ikiwa bado.
 
Jaribuni kiongozi.

Pana mtu alijaribu hii ya mchicha, sukari ikashusha sana, mpaka ikamlazimu kuanza kuipandisha. Ndio maana ni muhimu kuwa na vipimo. Ni kweli ni muhimu pia kuendelea kufuata masharti ya mtu mwenye kisukari...
Shukran sana Mkuu, tutakitafuta hicho kitabu cha Boaz Mkumbo
 
katika maisha yangu nimejitahidi kufuatilia sana hili tatizo la sukari/kisukari si kwakuwa mi ni mgonjwa ila kutaka kufahamu ufumbuzi wake u wapi na pia kuangalia fursa pia na kutaka kusaidia wanaonizunguka.

ila asilimia zaidi ya 95 dawa zote ni kusaidia kushusha sukari na kumpa mgonjwa matumaini na kumfanya afurahie maisha. ila changamoto kubwa niliyoiona hakuna ama hatujapata wataalamu wa kuweza kutusaidia kupata dawa ya kutibu kongosho ambapo ndipo tunapata tabu zaidi. Baadhi ya ndugu na rafiki zangu wa karibu wametumia dawa mbadala toka kwa madaktari wa dawa asili/dawa mbadala kwa muda sana ila wanapata nafuu ila dawa inakuwa haitibu tatizo husika zaidi kushusha sukari tuu. pia kunadawa nimewahi kutananayo inatoka somali kunamtu kaitumia na anadai kapona kabisa wasiwasi wangu ni je isije kuwa kapata nafuu theni tatizo likaja jirudia baada ya sikuu kadhaa.

Mtizamo wangu ni kuwa hizi dawa zipo sema si kwa watu wengi na matapeli na wataka pesa ndo wanatuchanganya, mfano mzuri ni ka tatizo la nyama za pua hospitali halitibiki na hata ukizikata nyama hizo zinaweza kurudi tena ila dawa mbadala zinaondoa kabisa na hazirudi tena namie nazijua pia
 
Tupo tuliojaribu juisi ya mchicha mbichi kushusha sukari?

Kilichohamasisha kuanzisha uzi huu ni uzoefu uliosikika kwa watu wawili.

1. Huyu yeye amesumbuka sana na sukari, mpaka katibiwa hospitali kubwa. Bado sukari ilikuwa na namba kubwa. Alichukua hatua mbili: kwa muda wa siku kadhaa alikuwa anakula nyama, kuku, samaki , mboga za majani na matunda yasiyo na sukari pekee, bila wanga. Hatua hii ilishusha sukari kwa kiasi fulani. Kisha alipokunywa juisi ya mchicha mbichi, ilishusha sana sukari kipimo cha nyumbani kikaonyesha 2 mmol/L; ikabidi kuanza kuipandisha mara moja; na wakasitisha kuendelea kutumia juisi ya mchicha mbichi.

2. Wa pili yeye aliumwa sana, na matibabu hayakumpa nafuu. Alipoenda zahanati kupimwa sukari, alikutwa nayo nyingi. Hakuwa na historia ya kisukari. Alikunywa bilauri moja ya juisi ya mchicha kwa siku tatu. Aliporudi zahanati, sukari ilikuwa imerudi kuwa ya kawaida. Na baadaye maisha yamerudi kawaida.

Watu wote hao wawili ni wa jinsi ya KE.
 
mfano mzuri ni ka tatizo la nyama za pua hospitali halitibiki na hata ukizikata nyama hizo zinaweza kurudi tena ila dawa mbadala zinaondoa kabisa na hazirudi tena namie nazijua pia
Ni dawa gani hiyo mkuu maana hili tatizo linasumbua watu wengi sana.
 
Mimi nina tatizo la sukari now natumia dawa Za hospital nishakunywa dawa Za asili kwa mihongo mingi sikubahatika kupata matokeo yoyote chanya na kikubwa gharama zake kubwa hela nyingi imepotea sana.

Mwisho nimeona nibaki na dawa Za hospital. Nimekula dawa hadi mchanga wa bahari unaloeka kuumwa kusikie tu kwa mtu na hii ndio inapelekea tunaliwa hela nyingi kwa shauku kutaka kupona.

Mimi mpk sasa siamini dawa ya kuponesha sukari. Hakuna tiba ya sukari Kama unatibu sukari Why pesa kwanza dawa ikiisha na lako limeisha sijaona mtu anatibu alafu hela baadae
 
Back
Top Bottom