lujoka
New Member
- Jun 8, 2024
- 1
- 1
Mapendekezo ya mabadiliko katika utaratibu wa uendeshaji wa mashauri yaliyo mahakamani. Watu wote wa kada mbalimbali, wa jinsia zote, wakubwa kwa wadogo wana haki sawa mbele za Mungu ambaye ndiye Jaji Mkuu aliye juu ya majaji wengine wote.
Mimi naamini pia kuwa mfumo wa mahakama katika nchi yetu ya Tanzania unalo kusudi la kuhakikisha kuwa kila mtu anayetafuta haki yake kupitia taasisi hii kubwa anapewa haki sawa bila ubaguzi wowote.
Katika kutimiza azma hii ninayo mapendekezo ya kuiomba taasisi hii itusaidie kufanya marekebisho kidogo katika utaratibu uliopo wa kusikiliza mashauli au kesi zilizopo mahakama za juu, mahakama za rufaa na zile zilizopo mahakama za chini na katika tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA).
Utaratibu unaofuatwa kwa sasa ni kwamba ikiwa wakili anayehusika na kesi iliyo katika mahakama ya chini na kama pia ana kesi Mahakama Kuu basi inapotokea tarehe za kuonekana katika mahakama hizi mbili zikagongana basi wakili atalazimika kuahirisha kesi iliyo katika mahakama ya chini ili aweze kuonekana mbele ya Jaji wa mahakama ya juu.
Hili ni jambo ambalo linamnyima haki ya kusikilizwa kwa wakati mtu aliye na kesi katika mahakama za chini. Hii ni kwa sababu hata ikitokea kwamba mahakama za chini zilipanga tarehe ya kusikiliza kesi na baadaye mahakama za juu zikapanga kesi katika tarehe hizohizo basi mahakama za chini zinapaswa kuahirisha kesi na kutafuta tarehe zingine.
Sina kusudi la kudharau Ukuu na umuhimu wa kesi zilizopo katika mahakama za juu. Maana ninatambua pia kuwa katika taratibu nyingi zilizopo duniani kipaumbele hutolewa kwa mdogo kumpisha mkubwa. Hata hivyo, ninaamini, kwa vile sijafanya utafiti, kwamba sababu mojawapo kubwa za kesi zilizo katika mahakama za chini na taasisi zingine zinazosikiliza mashauli ya watu kuchukua muda mrefu kwisha ni pamoja na kuahirishwaahirishwa kunakosababishwa na utaratibu huu wa mdogo kumpisha mkubwa.
Katika kutambua hili ndio maana utangulizi wangu ulianza kwa kuweka msisitizo wa kutoa haki sawa kwa watu wote wanaotafuta haki zao kupitia taasisi zilizowekwa kusimamia jukumu hilo la kutoa haki.
Mimi sioni umuhimu wa mahakama za juu kuweka kipaumbele kwa kesi zote zilizo katika mahakama za Juu ukilinganisha na zile zilizo katika mahakama za chini kwa sababu zifuatazo:-
1. Hawa wanadamu wenye kesi katika mahakama za juu ama za chini, kila mmoja yuko katika matatizo na anataka tatizo lake liishe kwa wakati ili aweze kuendelea na maisha mengine baada ya hukumu.
2. Mashauri ambayo yako katika taasisi ambazo hazipo chini ya mfumo wa mahakama moja kwa moja, mfano, Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) huwa ni wahanga wakubwa wa utaratibu huu maana haziwajibiki kuharakisha mashauri yao kwa udhibiti wa Mahakama Kuu. Hivyo haki za mdai au mdaiwa huweza kucheleweshwa kwa miaka mingi. Ipo mifano ya kesi zilizosikilizwa kwa zaidi ya miaka kumi!
3. Kwa kuwa kesi zinazopelekwa mahakama za juu zilizo nyingi huanzia kwenye mahakama za chini, lazima tukubali kwamba kwisha kwake kutakuwa na muda kidogo wa ziada kwa kusikilizwa rufaa yake. Ikiisha mapema katika mahakama za chini huo muda kidogo wa ziada katika mahakama za juu utakuwa hauna machungu zaidi kuuvumilia.
Mapendekezo yangu katika kulitatua tatizo hili ni kuiomba Mahakama Kuu ipange utaratibu ambao utalenga katika kuwapa usawa wa haki watu hawa. Haki hii itawahakikishia wahusika wote kuwa na muda wenye uhakika wa kusikilizwa kesi zao kwa wakati. Ili kwamba mtu ambaye ana kesi katika mahakama za chini anapokwenda kwenye tarehe ya kesi yake asiwe na kutarajia kuahirishwa kwa kesi yake kwa sababu tu ya wakili kuitwa kwenye kesi za mahakama za juu.
MAPENDEKEZO: Ninapendekeza kwamba zitengwe siku ambazo zitakuwa maalumu kwa kesi zinazo sikilzwa katika mahakama za juu na zile ambazo ni maalumu kwa kusikilizwa kesi za mahakama za chini. Katika siku hizo wakili ambaye anahusika katika mashauli ambayo yapo katika pande hizo zote atazitumia siku hizo katika kupanga kesi zake katika siku hizo maalumu.
Jaji wa mahakama za juu anaweza kupanga kesi katika siku yoyote na inapotokea wakili akitoa udhuru kwamba atakuwa na kesi katika siku za kesi kwa ajili za mahakama za chini basi Jaji huyo awe radhi kupendekeza tarehe nyingine tofauti na iwe katika siku zile ambazo ni maalumu kwa ajili ya kesi za mahakama za juu.
Hali kadhalika, mahakama za chini vivyohivyo zitazingatia siku zilizotengwa kwa ajili ya kesi za mahakama za juu kwa mawakili ambao wanahusika na kesi zilizopo mahakama za juu. Kwa mantiki hii, mahakama zinapotoa wito wa kwanza wa kufika mahakamani kwa wakili yeyote itabidi kuzingatia siku maalumu zinazohusika kwa ngazi ya mahakama inayotoa huo wito. Kwa njia hii tutaepuka kabisa zile sababu za kuahirisha kesi kwa sababu wakili amealikwa magakama za juu na hivyo kuwatendea haki wale ambao wanatafuta haki zao katika mahakama za chini.
MFANO: Ikiwa itaamriwa kwamba, mathalan, siku za Jumatatu na Jumanne ni siku maalumu za mahakama za juu na siku za Jumatano na Alhamisi ni siku maalumu za mahakama za chini basi mawakili walio na kesi katika mahakama za pande hizo mbili watapanga kesi zao zilizo mahakama za juu siku za Jumatatu na Jumanne na zile zilizo katika mahakama za chini watazipanga katika siku za Jumatano na Alhamisi.
NAWASILISHA.

Upvote
5