Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Naona kuna wito unatolewa kwa CHADEMA na baadhi ya watu kuwa chama hicho kisitushe maandamano hayo ya kudai haki kupisha maombolezo ya kifo cha Edward Lowassa.
Wanatumia kigezo kuwa Lowassa pia amewahi kuwa mgombea Urais wa chama hicho hivyo watakuwa wanadhulumu haki yake ya kuombolezewa. Naomba niwaambia Hawa watu mambo mawili.
(1) Lowassa naye aliwahi kudhulumiwa haki yake ya ushindi na hao hao wanaotoa wito kustopisha maandamano ya kudai haki. Hivyo kaburini Lowassa anashangilia bila shaka.
(2) Siku za maombolezo zilizotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni Tano (5) na zilianza tarehe 10 (Jumamosi) inayoisha leo tarehe 14/2/2025. Kuanzia kesho ni siku za kawaida na misiba mingi tu inaendelea ya kina Imani Madega, Dk. Kamara, Dk. Msabaha lakini yupo mkubwa mwingine tunajua yuko kwenye jokofu kupisha Lowassa ambaye bendera kwake najua itapepea siku Saba. Vifo vipo tu maana Kuna kizazi kimeruhusiwa kukatika.
Ushauri wangu CHADEMA andamaneni kama kawaida maana Msiba au mwili wa Lowassa hautakuwa Mwanza. Kama ni heshima za mwisho basi mlishatoa nyumbani Masaki na Karimjee. Ova!