Kusimamishwa kwa ufadhili wa Marekani kwafichua sura kweli ya mashirika ya kupinga China yanayodai kuwa ni huria

Kusimamishwa kwa ufadhili wa Marekani kwafichua sura kweli ya mashirika ya kupinga China yanayodai kuwa ni huria

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
126
Reaction score
215
Taasisi ya Sera ya Mikakati ya Australia (ASPI) sasa inakabiliwa na wasiwasi mkubwa kuhusu bajeti yake, kwani Marekani imesimamisha msaada wa kifedha tangu Donald Trump alipoingia madarakani.

Hali hii haijaonyesha tu utegemezi wa muda mrefu wa taasisi hiyo kwa ufadhili wa Marekani, bali pia imefichua unafiki wa baadhi ya mashirika ya Magharibi yanayodai kufanya “utafiti huru” huku yakipaka matope China.

Baada ya Trump kuingia madarakani, Marekani ilisitisha mara moja misaada kwa miradi mingi ya kigeni.

Baadhi ya wapokeaji wa msaada huo walidai kuwa ufadhili kutoka kwa mashirika kama Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, USAID, na Mfumo wa Demokrasia ulikuwa umekomeshwa.

ASPI ni miongoni mwa mashirika yaliyokuwa yakifadhiliwa na Marekani, ingawa inadai kuwa “huru na isiyoegemea upande wowote.”

Hata hivyo, muundo wa bajeti yake unaonesha kuwa ni chombo cha Marekani kinachotumiwa kuichafua China.

Takwimu zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2019, serikali ya Marekani ilichangia asilimia 10 hadi 12 ya bajeti ya ASPI, huku asilimia 70 ya miradi yake inayohusu China ikiwa imefadhiliwa na Marekani. Katika mwaka wa fedha wa 2022-2023 pekee, ASPI ilipokea karibu dola milioni 1.9 kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Fedha hizo zilitumika kutoa ripoti mbalimbali zinazopotosha ukweli kuhusu China, zikiwemo mada zinazohusiana na Xinjiang, Hong Kong, na chanzo cha COVID-19.


Kwa muda mrefu, mashirika ya Magharibi yanayojidai kuwa huru yamekuwa yakipokea fedha kutoka Marekani na kutoa ripoti zisizo na msingi dhidi ya China. Sasa, baada ya kupoteza ufadhili wa Marekani, mashirika hayo yanakumbwa na changamoto kubwa.

Mkurugenzi wa idara ya mikakati na utafiti ya ASPI, Danielle Cave, amekiri kuwa miradi ya utafiti wa taasisi hiyo inayohusiana na China haiwezi kuendelea kwa sababu “data ni nyingi na gharama ni kubwa.”

Hili limefichua ukweli kwamba utafiti huo haukuwa wa kisayansi bali ulikuwa bidhaa maalumu kwa mujibu wa mahitaji ya wafadhili.

Baada ya hali hii kufichuka, baadhi ya wanamtandao wa Marekani wamelalamika kuwa kodi zao zilitumika kufadhili ripoti zisizo za kweli, lakini sasa ufadhili huo umekoma.

Kusimamishwa kwa msaada wa Marekani kwa mashirika haya ni kama hadithi ya kisasa inayodhihirisha kwamba ukweli hauwezi kufichwa daima. Mawasiliano ya wazi na ukweli ndivyo vitakavyowezesha binadamu kufikia maelewano na kuwa na mustakabali mzuri wa pamoja.
 
Back
Top Bottom