Why Always Me-MARIO BALLOTELIEti kugegedwa kwangu kunakuja kujadiliwa jf ni fair eti? Kwani kuna shida gani eti mkuu.
Hili ndilo linalouma.. Mengine ya Kawaida tu..Lingine nikiwa mdogo kuna dada yangu mmoja alinisingizia nimemuibia mia yake aliweka mezani na mimi ni mtu pekee nilikuwepo humo ndani, alinikomalia kuwa nimeichukua akaanza kunipiga kadri ninavyokataa sijachukua ndivyo kipigo kinazidi, baadae nilipoona kipigo kimenielemea ikabidi nikubali kuwa nilichukua ila mimi pia nimeipoteza nilikokuwa ninacheza ndio kuniacha. Kesho yake asubuhi akiwa anapiga deki akaiona uvunguni mwa kitanda. Akaniita tena nikasema si unaona, mimi sikuchukua akataka kunishushia tena kipigo kwa kuogopa kipigo na fimbo za jana yake hata hazijapona nikasema niliidondosha mwenyewe baada ya kuchukua sikujua imedondokea hapo. Hili tukio huwa linaniumiza na kila nikikumbuka machozi yanadondoka ila nimepanga ipo siku nitamkumbusha mhusika najua ye kasahau.
Mkuu lile la kwanza haliumi? Walimu shule nzima wakujue kuwa wewe unajihusisha na ngono tena ukiwa shule ya msingi? Si kwamba sikuwa nasingiziwa hilo jambo ila hili liliniuma maana tuliwekwa hadi kitimotoHili ndilo linalouma.. Mengine ya Kawaida tu..
Aisee pole mkuuKwenye nyumba moja niliyopanga, mwenye nyumba alikuwa akiishi na mke wake, mtoto wao mdogo na mdogo wa baba mwenye nyumba wa kike umri kati ya 22 na 25. Yule mama mwenye nyumba alikuwa anaonyesha kila dalili kuwa anataka nimkune, nikawa napotezea, yeye akahisi yule wifi ndio kikwazo, kwamba akijua angemwambia kaka yake, alichokifanya ni kumwambia mume wake kuwa wifi yake huyo anajiletaleta kwangu, siku akipata mimba familia yao itapata aibu kwa kushindwa kumlinda, hivyo ni bora wamrudishe nyumbani kwa wazazi. Tofauti na alichotegemea, yule baba mwenye nyumba alinifuata na kunipa notice ya kuhama kisha akanieleza kwa masikitiko makubwa kuwa naonekana kijana mstaarabu kumbe mshenzi ninaetaka kumharibia mdogo wake, akanipa karatasi ya notice na kuniambia mkewe amemshauri amrudishe mdogo wake ila ni bora niondoke mimi mharibifu apangishe mtu na famili yake au mwanamke. Niliumia kusingiziwa huko, kodi ilipoisha nikawa tayari nishapata pakuhamia nikasepa.
Asante, ni vijimambo ambavyo vinafundisha na kukomaza akiliAisee pole mkuu
Maza nae akakosa mkunooo...Huyo maza ungemtafuta Private baada ya kuondoka...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwenye nyumba moja niliyopanga, mwenye nyumba alikuwa akiishi na mke wake, mtoto wao mdogo na mdogo wa baba mwenye nyumba wa kike umri kati ya 22 na 25. Yule mama mwenye nyumba alikuwa anaonyesha kila dalili kuwa anataka nimkune, nikawa napotezea, yeye akahisi yule wifi ndio kikwazo, kwamba akijua angemwambia kaka yake, alichokifanya ni kumwambia mume wake kuwa wifi yake huyo anajiletaleta kwangu, siku akipata mimba familia yao itapata aibu kwa kushindwa kumlinda, hivyo ni bora wamrudishe nyumbani kwa wazazi. Tofauti na alichotegemea, yule baba mwenye nyumba alinifuata na kunipa notice ya kuhama kisha akanieleza kwa masikitiko makubwa kuwa naonekana kijana mstaarabu kumbe mshenzi ninaetaka kumharibia mdogo wake, akanipa karatasi ya notice na kuniambia mkewe amemshauri amrudishe mdogo wake ila ni bora niondoke mimi mharibifu apangishe mtu na famili yake au mwanamke. Niliumia kusingiziwa huko, kodi ilipoisha nikawa tayari nishapata pakuhamia nikasepa.
Hapo sasa ningekuwa ni mshenzi na mharibifu kweli kama ambavyo mzee mwenye nyumba alivyo nifikiria. Sikutaka iwe hivyo.Maza nae akakosa mkunooo...Huyo maza ungemtafuta Private baada ya kuondoka...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hapo sawa mkuu...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Unajielewa sana!Hapo sasa ningekuwa ni mshenzi na mharibifu kweli kama ambavyo mzee mwenye nyumba alivyo nifikiria. Sikutaka iwe hivyo.
Daaaah nimekuona huruma sana kwnye hyo ya kupigwa kwa hela ambayo hujaibeba na mpaka ikabidi tu ukubali.....duuhh.
Binafsi nimewahi kusingiziwa mambo mengi sana.
Lakini sitasahau siku moja tupo darasan( darasa la sita) mwalimu wa kike alikua ubaoni anaandika somo la kiswahili sasa sisi tunacopy.
Mi nilikua na kaa nyuma ya darasa kama kiti cha tatu tokea nyuma..........mwalimu alikua amevaa kagauni kanaishia magotini.
Sasa mimi kunabaadhi ya maandishi ya chini ya ubao nilikua siyaoni na ni usawa aliosimama mwalimu huku akiendelea kuandika..........basi mimi nikawa napiga pozi kama nainama flani hivi kuangalia vizur maandishi,,,
Ghafla nikaskia sauti ya kike ((Mwalimu anakuchungulia huyu)))
Mi nikawa bize kuendelea kutoa macho kusoma kilichoandikwa ubaoni kwa pozi lile lile la kuinamia flan hvi ( sikustushwa na hiyo sauti wala sikujua kama yule dada anamaanisha ni mimi))
Mwalimu ile anageuka tu anakuta mtu nimejipinda kiupande upande afu nimeinama kwa kujikunja kinomaaaa,,,,,,afu ndo hapo na yule dada akadakia kwa sauti (( ni huyu flani)) darasa zima macho kwangu.
Nakabaki nimeduwaa na pozi lile lile na ticha akiangalia pozi langu basi hakutaka hata kuskia maelezo yangu ya kujitetea.......kipindi kikaishia hapo huku mim nikiongozana na ticha taratibu kwelekea ofisini akiwa amenikunja shati kwa nyuma.
Njiani alikua akitamka neno moja tu (( leo utanikoma we mtoto,,ntakuonesha ulichotaka kukiona kwnye gauni langu,,,na utanitajia jina la mama angu mzazi mpumbavu wewe))
Nilikula stick mpaka shule nzima ilikuja kujaa kwenye madirisha ya ofisini kuchungulia,,,,mana walianza kuskia sauti ya viboko tangu asubuhi wakat wanaingia class,,,sasa wanakuta mpka saa nne mda wa miogo viboko vinalia tu.........wakaona ataaa,,,,,hebu waje washuhudie kiumbe gan huyu anakula mboko mda wote huu...
Niliumia sana,,,,,,mpaka niliumwa nakumbuka
hako kadadaa ukakacha bila kipondo???
kwamba wewe ni baby yakeUlisingiziwa nini baby
Kumbe Ndo wewe ulosingiziwa kuwa una access na first reply ya kila threadNikikumbuka mwaka jana niliyosingiziwa hapa JF nabaki kusikitika na mengine kucheka yaani