SoC02 Kusitasita na hofu kunapelekea usiweze kufika katika hatma yako

Stories of Change - 2022 Competition

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,753
Reaction score
9,575
Awali ya yote ningependa kumshukuru Mungu kwa kunipa uhai na afya njema mpaka sasa ya kuweza kuandika Makala haya yenye kuleta badiliko kwa jamii hususani kijana na jamii inayotuzunguka katika mstakabali wa maendeleo yao.Pale watakapochukua hatua ya ziada kuondokana na hali ya kusitasita na woga wakutothubutu kufanya makusudio ama malengo yao.

Niende kwenye mada kuu ambayo ihusuyo hali ya kusitasita na hofu unaopelekea usiweze kufika katika mstakabali wa Maisha yako ama hatma ya Maisha yako hususani kwa jamii nzima.

HALI GANI HUTOKEA KWA MTU/WATU AMBAO WANAKUWA NA ROHO YA KUSITASITA KATIKA MAAMUZI YAO YA KUTEKELEZA KUSUDIO WALIOJIPANGIA?
Tutaangalia maeneo mbalimbali ambayo hufanya tusiweze kujikwamua katika Malengo yetu.

Tuchambue maeneo hayo kama ifuatavyo:-
  • Roho ya kusitasita inayokufanya uwe katikati
  • Hofu na woga unaokufanya usithubutu
1. Roho ya Kusitasita ya kutotekelza malengo yako kwa wakati
  • Kusitasita ni nini?
Ni hali ya kuwa katika mawazo mawili hata kushindwa kuchagua wazo moja la kulitendea kazi kwa wakati sahihi ulionao.
  • Mara nyingi roho hii huwakumba watu wa lika mbalimbali katika kusita kufanya maamuzi kwa wakati na kupelekea kushindwa kutekeleza kwa wakati malengo na azma ambazo walipanga kwa wakati huo na kufanya lile jambo kutofanyika kwa wakati. Ndiposa wanakuwa wamekwama na kutooona mstakabali mzima na muda kupotea bure. Roho hii ufanya mtu awe vilevile asiwe na maendeleo kabisa ambapo hupelekea kushindwa kufikia malengo yake na kuwa duni, kifikra, kiakili, na kimaisha pia. Mpaka anapogutuka anakuwa hana kitu chochote yuko empty na anafia hivyohivyo bila kuona mstakabali wa hatma yake
2. Hofu na woga unaokufanya usithubutu

Pengine tujiulize, kwa nini hali ya woga / hofu hujengeka katika nafsi zetu na kusababisha tusifanikiwe katika yale malengo tuliyojiwekea. Mojawapo ya sababu nilizokwisha elezea hapo mwanzo :

A: kuogopa kuthubutu : kuogopa kutekeleza yale ambayo uliyapa kipaumbele kuyafanya kwa wakati fulani na hukuweza kufanya. Matokeo yake umebaki kwenye hofu ambayo inakufanya uwe duni kifikra, kiakili na duni wa maisha kiujumla umebaki kuwashangaa wengine wanavyofanikiwa nawe unabaki kuwa vilevile na miaka inasonga wala hairudi nyuma umebaki mtu wa huzuni ambao hukupa woga fulani pengine labda kwa mambo fulani yaliyotokea kwako ndo yamepelekea ushindwe kuthubutu kutekeleza, Hebu jisemee moyoni kuwa UNAWEZA KATIKA YEYE AKUTIAE NGUVU [MUNGU aliyekuumba] NA JENGA IMANI YA USHINDI NDANI YAKO. Hukujiumba bali uliumbwa uushangaze ulimwengu kwa yale utakayojinenea moyoni mwako na kuyapa taswira ndipo utendeka katika uhalisia huu wa duniani.

B: Nia na wazo jipya ulilojijengea katika fikra zako kwamba siwezi:
Unaponuia na kuwa na wazo jipya lililojijenga katika fikwa zakolitaweza kutimia endapo utachukua hatua ya ziada ya kuthubutu kulitendea kazi. Ukitaka uyaone matunda ya mawazo, au fikra zako anza kufanyika kazi katika kuiendea ono lako na kuwa mtu mwenye utafiti na mdadisi wa jambo ambalo unataka litokee kwako, kama hutashindwa kuwa mdadisi basi hutaweza kuiendea ndoto iliyopo machoni pako ama moyoni mwako. Sayari yetu imejaa vitu mbalimbali ambavyo viliundwa, vikatokea wako watu ambao walikuwa wadadisi wa mambo na walikuwa watafiti sana; ambao waliona ndoto zao na kuchukua hatua ya ziada kuziendea ndoto zao ambazo zimeleta matunda kwenye sayari yetu; pengine kwao tumeweza fanikiwa kutumia vitu vigunduzi vyao; kwani tunafurahia matunda yao kwa sasa ambayo yamefanya urahisi kwetu.

Hebu tuwaangalia hao wagunduzi wachache ambao waliamka fikra zao na kufanya mambo makubwa ambayo mpaka sasa tunayafurahia na kutumia.

Wagunduzi hao ni:-
1. Isaack Newton
2. James Watt

1. Mgunduzi Isaack Newton aliyegundua Nguvu ya Uvutano.

Picha kwa hisani ya mtandao

  • Wagunduzi wengi wa kiutafiti walianzia kwenye wazo dogo sana la kutafiti wa kitu katika fikra, mawazo yao ambayo yalipelekea kuundika kwa kitu kamili; baadhi yao hawa wagunduzi walianzia kwenye mambo ya kijamii, kisiasa, na kiuchumi na mambo ya kisayansi pia. Kwa mfano: mgunduzi Isaack Newton aliyetokea nchini Uingereza yeye aliweza kugundua na kuelewa Nguvu ya uvutano’ (Acceleration due to gravity); wakati akitafiti na kufikiria jinsi gani unaweza kurusha jiwe au kitu kizito juu angani; lile jiwe/tufe likaanguka halikubaki hewani, alishangaa sana kwanini lisiende juu au kubaki hewani tu ndipo aliona uhusiano uliopo kati ya nguvu ya sayari ya kuvuta vitu; Ule mwendo wa kitu unabakia hadi usukumwe kutoka nje. Newton alipewa uwezo huo na Mungu kwani ndani yake kulikuwa na uwezo wa uungu alikuwa mtafiti na mdadisi wa mambo hakukaa na kitu ndani yake bila kukifanyia kazi. Na hatimaye ndoto zake zilifanikiwa.


    picha kwa hisani ya mtandao


  • 2. Mgunduzi mwingine aliyegundua Injini ya mvuke : James Watt anayetambulika kama mgunduzi aliyebadilisha muundo wa maisha ya wanadamu na kuleta mafanikio makubwa kisayansi; James Watt aligundua injini inayozuia upotevu wa mvuke wa injini za maji; aliwezesha Uingereza kuingia katika mapinduzi ya viwanda mnamo mwaka 1775. Alitafuta njia mbadala ya kuondoa tatizo lilikuwepo kwa kurekebisha mapungufu ya injini ya New common iliyokuwepo wakati ule na kukamilisha ili isiweze tena kupoteza mvuke. Alipofanikiwa kufanya hivyo; ndipo injini hizo zikaweza kutawanywa takribani kila mahali. Kuwezesha kuundwa viwanda kulitegemea kuwepo au upatikanaji wa eneo ambako rasilimali ya kutumia injini ni nyingi hasa maji na makaa ya mawe. James Watt alilitambua hilo ndipo akagundua tatizo lililokuwepo wakati ule. Ugunduzi ni kitu kinachopenya na kupinda bila shida hivyo inaweza kuingia katika nafasi isiyo na hewa (vacuum) na kama mawasiliano yataundwa kati ya mvuke huo na kipokea cha mvuke. Ili kuwa na kifaa kingine (exhaust vessel) itajijaza mle ndani hivyo isipoteze joto bila kupunguza joto la kipokea chake. Ilikuwa ni ugunduzi wa Vacuum kulinda joto la chombo. James Watt aliweza pia kutengeneza viunganishi vya aina nyingine; mfano msukumo wa mvuke huo katika mikanda ya mzunguko (pulleys). Ugunduzi huo unaleta mafanikio makubwa badala ya kutumia farasi kusukuma gari tunatumia injini ya mvuke kusukuma gari na kuendeka kirahisi pasipo kutarajia.
Ni vyema tukaenzi ugunduzi huu na vilevile hata sisi tukawa wabunifu na wagunduzi wa vitu. Hawa wagunduzi waliweza kufanya kitu kikatoka kwa zile jitihada na bidii zao; iweje hushindwe, la hasha tunaweza kugundua kitu na kikatendeka. Nisingelipenda kuwaongelea/wazungumzia watafiti na wagunduzi wa nje ya nchi yetu. Hata hapa tuna watafiti waliokuwa na bidii na jitihada za hali ya juu kuweza kugundua kitu kikafanyika na kuleta manufaa kwa jamii yetu. Mfano wa watafiti wetu jopo la wasomi wa Chuo cha UDSM walioweza kuunganisha mtaala wa Utafsiliwaji wa lugha ngeni katika Kompyuta na kuweza kuipitisha lugha yetu ya Kiswahili kuingia katika Program za mtandao wa tovuti (internet) ambayo imepelekea kueleweka zaidi kwa jamii inayojua lugha ya Kiswahili na kutumika kirahisi katika kompyuta na visimbuzi vyetu. Na kutufanya tuweze kuwasiliana kiurahisi kwenye mitandao yetu hususani wale wanaoijua lugha yetu ya Kiswahili.

HITIMISHO LANGU

Kusitasita ni ugonjwa ambao uko kwenye mfumo wa fahamu ambao unakudidimiza au unatudidimiza tusione hatma zetu na hofu na mashaka utukumba na kufanya tushindwe kutimiza yale tuliojipangia kwa wakati huo, tunakuja kugutuka wakati kweupe na jua limechomoza, ndipo hapo sasa tunakuwa hatuna jinsi kwani tunafunua shuka wakati wa mwanga kuwepo.

Rafiki yangu na mpendwa msomaji wa Makala yangu uenda nawe unao ugunduzi ila bado hujajitambua, na wala huna rasilimali mali za kuweza kuingiza kwenye ubunifu wako na kutendea kazi; usikate tamaa kirahisi rahisi tegemea kuwa ipo siku utavuka na utaweza pata rasilimali hizo za kuweza kutekekeleza kusudio lako. Waswahili wanasema mambo mazuri hayaji kwa haraka vuta Subira ila wakati unavuta subra, anza kulifanyia kazi ono/ndoto yako usiwe na roho ya kusitasita kwani huleta umaskini katika mstakabali wa kufikia hatma yako. Nitafurahi sana endapo msomaji wangu utachukua hatua ya kuthubutu na kulitendea kazi ndoto zako

Marafiki zangu naomba mnipigie kura kwa wingi kwenye kitufe cha kupigia kura hapo mwisho wa bandiko langu,
Ndimi Ladyfurahia
 
Upvote 18
 
Nipo dada yangu. Ulipotea mno. Nimesoma uzi unatukumbusha kujaribu au kufanya kile tunacho waza kwa maana kinaweza kuwa njia ya kugundua kitu kipya kitakacho tupa kujifunza au kutupa uzoefu wa jambo husika katika maisha yetu
 
Hongera kwa andiko zuri.

#MaendeleoHayanaChama
 
Asante ndugu mleta mada, kwa kiasi kikubwa itafungua fikra za vijana wengi haswa linapokuja swala la kujikwamua kutoka katika umaskini, mara nyingi tunapata njia mbalimbali lakini udhubutu tunakosa na tunaendelea kubaki katika lindi la umaskini.

Tunashukuru kwa majukwaa kama haya ingawa kwa bahati mbaya wanao bahatika kusoma makala kama hizi ni wachache sana, hata hivyo wengi wetu tunapata mwamko mpya.
 
Iko sawa ndugu, pia karibu usachi Kaka Ibrah ili ujifunze na kunipigia kura kupitia machapisho yangu huko.
 
kabisa pendaelli kwani tukijitambua tu kwa tunaweza basi tuttatoka katika lindi la fikra za kimaskini
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…