Mimi nimesikitika sana watz wenzangu je nyinyi mmelipokeaje? Ishu ni kwamba wahadhiri walikuwa wanamadai ya msingi kwa uongozi wa chuo hicho kilichokuwa na sifa zamani lakini sasa kimegeuka secondary ya kata. jambo la kwanza lililowauma wahadhiri hao ni chuo kusitishwa kudahili wanafunzi wapya kutokana na chuo kukosa ithibati iliyokwisha muda wake, pili Viongozi wa chuo hicho mkurungenzi wa fedha na utawala, Mkuu wa chuo na Mkurugenzi wa mafunzo wote hao hawana sifa zinazotakiwa na baraza la elimu ya ufundi NACTE mfano, Mkuu wa chuo (Principal) anatakiwa kuwa na PHD, Mkurugenzi wa mafunzo (DOS) anatakiwa kuwa na PHD, Mkurugenzi wa fedha na utawala anatakiwa kuwa Lecturer Mwenye masters na awe ametoa maandiko matatu (should publish) lakini wote hao hawana hizo sifa je kuambiwa ukweli ni kosa? pia wahadhiri walikuwa wanalalamikia nyongeza na malimbikizo ya mishahara yao zaid ya miaka kumi nyuma pamoja na ubaguzi na manyanyaso ya viongozi hao wasiojua utawala wa kidemokrasia wala sheria. Sasa wahadhiri wamefukuzwa na inasemekana wameajiri wahadhiri wengine wasio na sifa mfano, ukienda pale chuoni kuna dada amaajiriwa amesoma chuo miaka minne (4years instaed of 3 years sababu carry forwad) sas huyu anasifa au anasifiwa? wahadhiri hao kama ukitaka kujua ukweli wa mambo walisha wahi kumuandikia barua waziri mkuu tangu mwaka jana juu ya matatizo ya chu chao lakini hakuna la maana lililofanyika, na juzi to mwezi wa saba walimuandikia mkuu wao wa bodi ya magavana report yenye maovu na aibu ya viongozi wa chuo pamoja na matatizo ya chuo ili kupata suluhu lakuni kilichofuatia ni kutafuta watu waliotafuta nyaraka zilizoambatanishwa kwenye report hiyo na kuwapatia barua za kujiereza. sababu zilizowasitisha kazi wahadhiri hao eti ni kutotii amri ya uogozi wa juu, je utatii vipi uongozi kama uongozi wenyewe ni wa kidharimu? majungu, undugu, kulindana na kuteteana tokea Wizarani mpaka chuoni? JAMANI NASIKITIKA KUONA WASOMI WANARUDI MTAANI WAKATI BADO TAIFA NI CHANGA NA LINAHITAJI WATU WENYE KUPIGANIA HAKI KAMA WAO. MIMI NAWAPA POLE NA NASEMA FUATILIENI KESI HIYO UKWELI UBAINIKE. SOLIDARITY FOREVER!