A
Anonymous
Guest
Mimi ni mkazi wa Kawe, Dar es Salaam, nina imani Nchi yetu kwenye Sheria za ardhi kuna maeneo specific kwaajili ya ujenzi wa Makanisa na Misikiti, kwa habari za Misikiti wanajitahidi sana na tunawapongeza ila kwa makanisa especially haya ya Manabii jamani ni changamoto especially Kawe jamani.
Kuna Manabii kibao ila Nabii mkubwa ni Mwamposa ambaye anafanya shughuli zake katika hili eneo la Serikari la Tanganyika Peckers. Anapofanyia saizi panaendelea ujenzi wa nyumba za NHC kama sikosei sasa anatakiwa ahame.
Kwa hiyo Serikali imeamua kumpa eneo hapahapa Kawe Tanganyika Peckers ila safari hii wamemsogeza karibu kabisa na makazi ya Watu. Ubaya ni kwamba walipomleta kuna shule nne ukiachana na makazi ya Watu, shule hizo mbili ni za Serikali na za private mbili.
Watu wote wanajua ukubwa wa Mwamposa na wingi wa Watu alionao pamoja na kelele ambazo zinatoka hapo alipo, sasa mbaya zaidi wanamleta kwenye makazi ya Watu na bila hata Serikali kujali lolote.
Je, Serikali haijali Wananchi kiasi kwamba haifikirii shule wanazosoma Watoto? Pale palikuwa na Uwanja wa Mpira ambao Watoto wa Shule walikuwa wanacheza ila Mwamposa kachukua pote na ukizingatia eneo lina Heka zaidi ya 10, kweli hata kama walishindwa kumpa hata Heka 3 tu mbali kidogo na makazi ya Watu?
Pili wakazi wa Kawe hatuna barabara za mtaa, yaani ni mbovu hasa, kwahiyo Wananchi wakajitengenezea barabara inayopita hapo Tanganyika Packers, lakini kaja Mwamposa tena kwa mabavu ameziba barabara kisha anakwambia tukapambane na Serikali, tumekimbilia kwa Serikali za Mtaa wanasema suala hilo limefanywa na wakubwa, hivyo wao hawawezi kusema lolote.
Pale Mwamposa alipo sasa pana mazingira mabovu mno ana Watu wengi na choo havitoshi kwa hiyo hata ukipita pananuka sana vinyesi sasa Serikali kwanini iruhusu mtu huyu aje kwenye makazi ya Watu?
Yule baba ana hela anaweza nunua popote na kujenga kwanini aje kwetu na kufanya ubabe huu. Plus huku mtaani tayari kuna Makanisa mengine manne ya Manabii wengine na mitume, yaani ni mateso mbona hatuna pa kusemea.
Soma pia Je, Mamlaka iliyomuhamishia Mwamposa nyuma ya Shule za Feza, Ukwamani Secondary na Kawe B ina Akili sawa sawa?