Kusoma computer bongo kunabebwa na wanaokufundisha

Kusoma computer bongo kunabebwa na wanaokufundisha

Joined
Jan 9, 2024
Posts
3
Reaction score
5
Vitu ambavyo tunafundishwa huko Machuoni, mahali ambapo tunalipia ada zaidi ya milioni 1 iwe kwa mihula michache au mingi, lakini ukweli acha tuongee. Unakuta mtu anaenda kusomea course labda ya IT, ila vitu ambavyo anafundishwa si deep ya IT kama inavyotaka. Ifukunyuliwe inaguswa tu juu, labda kwenye upande wa maana ya IT, inavyofanya kazi, content zake za ndani, na mambo mengine madogo madogo.

Shida sio mfundishaji anaekufundisha iyo course, shida ni yeye mfundishaji alivyofundishwa na ndo anavyokufundisha wewe. Kikubwa ukienda chuoni, usije uka base sana na chuo, ukadhani kila kitu utapata huko kuhusu course unayoenda kusomea. Ukiwa unaendelea na chuo, hakikisha na wewe unapata mahali pa kukuendeleza kutokana na iyo course yako uliyochagua. Yaani ujifunze vitu vya juu tofauti na unavyofundishwa chuoni.

Mwisho.
 
Chuo siyo shule, mwalimu anamasaa manne tu ya kukuonyesha njia wewe una masaa sita ya kujisomea na masaa kadhaa(nimesahau idadi) kwaajiri ya mazoezi/practising tu. Elimu ni bahari mwalimu awezi ogelea bahari yote nenda kaogelee popote baharini kwaajiri ya ubora wa elimu yako.
 
Back
Top Bottom