Kusoma Nje ya Nchi: Is It Worth it?
If you have traveled out to obtain another degree, could you please share your experience around the points below:
- What major difference did you notice in the education system that you think should be implemented in the Tanzanian education sector?
- Je? utawahimiza wanafunzi kuchukua mkopo kwa ajili ya kusoma nje ya nchi?
- Kusoma nje ya nchi kuliku badilishaje kama mtu? na una hisi ilikuwa na athari gani ya moja kwa moja kwenye maendeleo yako binafsi ya ki kazi na ki maisha.
Let's hear from you...
Nitatoa mfano wa Marekani, kwa sababu ndipo niliposomea.
Nilipokuwa nasoma undergraduate, kulikuwa na somo moja elective la Philosophy. Halikuwa la lazima kwa course yangu. Nililichagua kwa sababu napenda Philosophy.
Sasa basi, kuanzia siku ya kwanza, kabla ya kujuana sana na Profesa, sikungojea sana kuanza ubishi wa kifalsafa.
Badala ya kubishia mada ya darasani, nikaanza kulibishia somo lenyewe, kwamba somo limeitwa Philosophy, lakini katika materials tunazungumzia Western Philosophy tu. Yani hakuna hata topic moja kuzungumzia falsafa za Asia au Africa, ilikuwa Wagiriki na kwenda mbele kwenye Western Philosophy.
Profesa akajitetea kwamba hivyo ndivyo somo lilivyo, na hata akitaka kufundisha nje ya hapo, hana ujuzi nako.
Profesa wa somo alikuwa mtu tofauti sana na mimi, alikuwa mzungu, mimi muafrika, alikuwa conservative, mimi nilikuwa liberal, alikuwa mzee, mimi nilikuwa kijana, alikuwa a relatively wealthy published judge, mimi nilikuwa mwanafunzi kutoka Afrika.
Basi kutoka hapo, kila siku darasani ubishi kwenda mbele. Yani huyu Kiranga unayemuona hapa ana afadhali, darasani ilikuwa Kiranga++. Mpaka siku nyingine nikaona nina dominate sana darasa. Nabishana na Profesa, namtajia vitabu, falsafa, nazama ndani sana.
Kuna dada mmoja mpaka akaniuliza, hivi, ule ubishi unaofanya darasani, ni kweli unaamini vile au unafanya figisu za kuchangamsha darasa tu? Nikamwambia naamini kweli.
Basi, siku ya mtihani wa mwisho ikasogelea, nikawa najiandaa kwa mtihani.
Nilikuwa maktaba ya chuo nasoma, nikaona email imeingia kutoka kwa huyu Profesa. Ananiambia usije kwenye mtihani wa mwisho.
Nikasema loooh salaaaleh, hapa ndipo napata ujira wa ubishi wangu wa kila siku darasani. Profesa ananifelisha kabla sijaingia kwenye chumba cha mtihani.
Nikamuuliza Profesa, vipi? Kwa nini nisije?
Akasema ushapasi mtihani kwa coursework yako.
Nikasema sasa nimepasi kwa alama gani?
Akaniambia A+, zile nondo ulizokuwa unatoa darasani si nondo za degree ya kwanza (undergraduate). Zile ni nondo za degree ya pili.
Jambo hili lilinifanya nifikiri sana kuhusu uhuru uliopo katika mfumo wa elimu wa Marekani.
Nikajiuliza sana, kama ningekuwa katika vyuo vyetu vya nyumbani, je, ningeweza kudiriki kubishana na Profesa vile? Je, Profesa angeniachia nibishane naye vile? Je, angeweza kunipongeza kwa ubishi wangu kwa kuwa umebeba mantiki? Je, angeweza kunipa A+ na kuniambia nisije katika mtihani wa mwisho?
Profesa yule alikuja kutaka kuwa rafiki yangu sana, alitaka niende kuwa msemaji katika mikutano yao na kujenga network zaidi.
Kuna faida nyingi za kusoma nje, kuona dunia, kujenga network (kuna mdogo wangu alipata kazi Dar, kwa kampuni ya Wa South Africa, kwa kuwa tu waliona amehitimu University of Cape Town, chuo ambacho wao wanaamini ni "Harvard of Africa".
Ila pia, kusoma nje ni gharama kubwa, kama suala la gharama linakuwa mzigo mkubwa, mtu anaweza kuanza kusoma nyumbani, halafu akajiendeleza kusoma nje hata mitandaoni tu, siku hizi teknolojia inaruhusu.