Dr am 4 real PhD
JF-Expert Member
- Jun 30, 2016
- 11,640
- 24,066
If you have traveled out to obtain another degree....?Sasa kama mtu kasoma degree nje, atawezaje linganisha na elimu ya degree ya ndani ambayo hajaisoma?
If you have traveled out to obtain another degree....?
Siku zote tunajifunza Kwa walio fanikiwaa...Kwa hiyo unataka watu walinganishe mazingira ya kupata diigrii ya kwanza nchini na digrii ya pili ughaibuni?
Hapo kwenye kusimamia miradi nimepapenda...Kwa failures bora ubaki hapa kuliko kusoma vyuo vya global education link
Ila kama ulifauli vizuri na una uwezo nenda piga hizo toefl, ielts, sat etc nenda.
Usikope kwenda kusoma.
Kama ulifeli na nyumbani hela zipo kasome nje ya nchi, urudi usimamie miradi
Nani ambaye atakusikiliza? Sisi mpaka tuliandika proposal kabisa na kuipeleka kwa wahusika kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha elimu ya msingi na Sekondari kwa case studies ambazo tuliziona kule zikifanyika laivu na kufanikiwa sana. We never heard anything back. Nobody gives a damn na kila waziri anayekuja anakuja na mawazo yake anavuruga. Anakuja mwingine naye anavuruga. Hakuna lengo-mama la elimu yetu na kuona kama inaendana na dunia inakoenda miaka mitano-ishirini ijayo!Siku zote tunajifunza Kwa walio fanikiwaa...
Watu ambao wana exposure ya kusoma mbele Kuna vitu wanaweza kusaidia kuboresha education system yetu...
Studying abroad gives you access to latest technologies, facilities, resources, reputed academics, peers as well as exposure to what may be pioneering discoveries and research......
Nitatoa mfano wa Marekani, kwa sababu ndipo niliposomea.Kusoma Nje ya Nchi: Is It Worth it?
If you have traveled out to obtain another degree, could you please share your experience around the points below:
- What major difference did you notice in the education system that you think should be implemented in the Tanzanian education sector?
- Je? utawahimiza wanafunzi kuchukua mkopo kwa ajili ya kusoma nje ya nchi?
- Kusoma nje ya nchi kuliku badilishaje kama mtu? na una hisi ilikuwa na athari gani ya moja kwa moja kwenye maendeleo yako binafsi ya ki kazi na ki maisha.
Let's hear from you...
Kuna muda unawaza labda wazaliwe malaika kutuongoza....Nani ambaye atakusikiliza? Sisi mpaka tuliandika proposal kabisa na kuipeleka kwa wahusika kuhusu jinsi tunavyoweza kuboresha elimu ya msingi na Sekondari kwa case studies ambazo tuliziona kule zikifanyika laivu na kufanikiwa sana. We never heard anything back. Nobody gives a damn na kila waziri anayekuja anakuja na mawazo yake anavuruga. Anakuja mwingine naye anavuruga. Hakuna lengo-mama la elimu yetu na kuona kama inaendana na dunia inakoenda miaka mitano-ishirini ijayo!
Mkuu,Kwa failures bora ubaki hapa kuliko kusoma vyuo vya global education link
Ila kama ulifauli vizuri na una uwezo nenda piga hizo toefl, ielts, sat etc nenda.
Usikope kwenda kusoma.
Kama ulifeli na nyumbani hela zipo kasome nje ya nchi, urudi usimamie miradi
Well said, Kuna professor Y. Bwatwa the Late,Nitatoa mfano wa Marekani, kwa sababu ndipo niliposomea.
Nilipokuwa nasoma undergraduate, kulikuwa na somo moja elective la Philosophy. Halikuwa la lazima kwa course yangu. Nililichagua kwa sababu napenda Philosophy.
Sasa basi, kuanzia siku ya kwanza, kabla ya kujuana sana na Profesa, sikungojea sana kuanza ubishi wa kifalsafa.
Badala ya kubishia mada ya darasani, nikaanza kulibishia somo lenyewe, kwamba somo limeitwa Philosophy, lakini katika materials tunazungumzia Western Philosophy tu. Yani hakuna hata topic moja kuzungumzia falsafa za Asia au Africa, ilikuwa Wagiriki na kwenda mbele kwenye Western Philosophy.
Profesa akajitetea kwamba hivyo ndivyo somo lilivyo, na hata akitaka kufundisha nje ya hapo, hana ujuzi nako.
Profesa wa somo alikuwa mtu tofauti sana na mimi, alikuwa mzungu, mimi muafrika, alikuwa conservative, mimi nilikuwa liberal, alikuwa mzee, mimi nilikuwa kijana, alikuwa a relatively wealthy published judge, mimi nilikuwa mwanafunzi kutoka Afrika.
Basi kutoka hapo, kila siku darasani ubishi kwenda mbele. Yani huyu Kiranga unayemuona hapa ana afadhali, darasani ilikuwa Kiranga++. Mpaka siku nyingine nikaona nina dominate sana darasa. Nabishana na Profesa, namtajia vitabu, falsafa, nazama ndani sana.
Kuna dada mmoja mpaka akaniuliza, hivi, ule ubishi unaofanya darasani, ni kweli unaamini vile au unafanya figisu za kuchangamsha darasa tu? Nikamwambia naamini kweli.
Basi, siku ya mtihani wa mwisho ikasogelea, nikawa najiandaa kwa mtihani.
Nilikuwa maktaba ya chuo nasoma, nikaona email imeingia kutoka kwa huyu Profesa. Ananiambia usije kwenye mtihani wa mwisho.
Nikasema loooh salaaaleh, hapa ndipo napata ujira wa ubishi wangu wa kila siku darasani. Profesa ananifelisha kabla sijaingia kwenye chumba cha mtihani.
Nikamuuliza Profesa, vipi? Kwa nini nisije?
Akasema ushapasi mtihani kwa coursework yako.
Nikasema sasa nimepasi kwa alama gani?
Akaniambia A+, zile nindo ulizokuwa unatoa darasani si nondo za degree ya kwanza (undergraduate). Zile ni nondo za degree ya pili.
Jambo hili lilinifanya nifikiri sana kuhusu uhuru uliopo katika mfumo wa elimu wa Marekani.
Nikajiuliza sana, kama ningekuwa katika vyuo vyetu vya nyumbani, je, ningeweza kudiriki kubishana na Profesa vile? Je, Profesa angeniachia nibishane naye vile? Je, angeweza kunipongeza kwa ubishi wangu kwa kuwa umebeba mantiki? Je, angeweza kunipa A+ na kuniambia nisije katika mtihani wa mwisho?
Profesa yule alikuja kutaka kuwa rafiki yangu sana, alitaka niende kuwa msemaji katika mikutano yao na kujenga network zaidi.
Kuna faida nyingi za kusoma nje, kuona dunia, kujenga network (kuna mdogo wangu alipata kazi Dar, kwa kampuni ya Wa South Africa, kwa kuwa tu waliona amehitimu University of Cape Town, chuo ambacho wao wanaamini ni "Harvard of Africa".
Ila pia, kusoma nje ni gharama kubwa, kama suala la gharama linakuwa mzigo mkubwa, mtu anaweza kuanza kusoma nyumbani, halafu akajiendeleza kusoma nje hata mitandaoni tu, siku hizi teknolojia inaruhusu.
Elimu za mbele Zipo good ila za bongo ni mbovu maana zinafundishwa na walimu waliofeliNdiyo.
Kuna faida nyingi sana. Exposure. Kuiona dunia ilivyo na jinsi wenzetu walikofikia. Pia unaona elimu ya wenzetu ilivyo mpaka unatambua kuwa hawajaendelea kwa kubahatisha bali wamewekeza sana kwenye elimu. Na ualimu ni taaluma inayoheshimika sana kiasi kwamba siku Mpwayungu Village akienda kule itabidi atubu na kuwaomba msamaha walimu wote.
Ni vizuri zaidi ukipata full scholarship wewe kazi yako inabaki kupiga kitabu tu na ukiamua kufanya kazi basi iwe ni kwa hiari yako kwa ajili ya kupata vijisenti vya ziada.
Kama una mpango wa kurudi home baada ya masomo pengine siyo wazo zuri kuchukua mkopo maana hata ukirudi na degree yako nzuri nobody cares huku nyumbani labda ubahatishe kwenye international NGOs/organizations ambako malipo kidogo ni nafuu. Vinginevyo itakubidi uwe na connection nzuri bila ya hapo utakutana na vizee vya vitengo huko vimekakawana vitakufanyia figisu na hata kukurestisha ini pisi ukizubaa.
Na ukiwa mtundu unaweza kuja na wazo zuri la kujiajiri japo itakulazimu ujiandae kwa vipingamizi na ukiritimba utakaokutana nao. Ni vyema ukienda kusoma mambo ya afya, kompyuta, uhandisi, uchumi, sheria na mambo yanayohusiana na finances.
Oooh...na mademu wa kizungu unawachakaza unavyotaka na kulipiza kisasi japo kidogo kwa waliyofanyiwa mababu zetu akina Kijenketile Ngwale, Mkwawa na Mangungo...[emoji16][emoji16][emoji16][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
Elimu, elimu, elimu....hakuna siri nyingine ya maendeleo ya kweli!
View attachment 2471248