Kusomana kwa mifumo BRELA NA TRA

Kusomana kwa mifumo BRELA NA TRA

ThnkingAloud

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
546
Reaction score
564
Baada ya serikali kuanza utaratibu wa kuhakikisha mifumo yake inasomana kuna utaratibu mzuri unaohakikisha kuwa ukishasajiri kampuni ile namba yako ya usajiri ndiyo namba hiyohiyo kwa ajili ya mlipa kodi. Yaani ni namba hiyohiyo ya TIN Registration kwa sababu mifumo inasomana. Hili ni jambo jema sana na ninawapongeza kwa hilo.

Changamoto inalijitokeza ni kuwa TRA wao wanadhani (na wakati mwingine hata BRELA) ukishapata usajili wa BRELA na TRA tu basi unaanza biashara immedately. TRA wanaanza assessment ya kodi ya mapato, PAYE, n.k. kwa mwezi na BRELA baada ya miezi kumi na mbili wanadai uwapelekee Audited Financial Statements kupitia kwenye mfumo wao online yaani ORS wakati unafanya filing ya Annual Return. Sasa Audited Financial Statements utazipata wapi wakati hata biashara hujaanza? Hata TRA filing of NIL Return haina maana mpaka kampuni ianze operations. Utakuta umerundikiwa faini kubwa kwa ajili ya kutokufaili NIL Return tu ya kodi ya mapato na PAYE. Ili isiwe tabu mtu anaamua kuitelekeza hiyo kampuni inayodaiwa mabilioni ya faini wakati hata operations haijaanza bado inadunduliza mtaji.

Kumbe on the ground kinachotokea siyo hicho hata kidogo. Ukweli ni kuwa unakuwa bado una-mobilize resources za aina mbali mbali kubwa ikiwa ni rasilimali fedha. Hujaanza biashara kabisa. Nashauri baada ya usajili kampuni ipewe muda wa maandalizi kabla ya haya kuanza kufanya kazi.

Namuomba Prof. Kitila Mkumbo alichukue hili ili serikali iweze kufanya marekebisho kwa kuwashauri TRA na BRELA kuendana na what is on the ground. Wabadili automation ya mifumo yao inavyosomana inayopelekea hii changamoto.

Nimemuona waziri kwenye press conference na waandishi wa habari leo na mimi ndiyo mchango wango huo.
 
Kitila Mkumbo
 
Na imani serikali sikivu itazingatia na kulifanyia kazi hili la mtoa mada maana ni janga la kidogo.
 
Back
Top Bottom