Kustaafu kucheza soccer kwa kroos

Kustaafu kucheza soccer kwa kroos

Extrovert24

Senior Member
Joined
Jun 23, 2022
Posts
144
Reaction score
211
Wakuu mambo ni vipi wapenzi wa kabumbu.
Huyu Jamaa ni kama Bado anaubonda mwingi sana, kwanini asingeendelea kupiga mbungi??
20240602_105420.jpg
 
UEFA 6, world cup 1 na domestic cup ameshinda za kutosha, Hana tena cha kupigania...by the way timing ndiyo Kila kitu, kachagua muda muafaka anaondoka lakini ana furaha ya kombe , ni kumbukumbu nzuri mno.
 
Kajamaa kana misimamo hako.Kanadai hakuna jipya tena wala pesa haikazuzui tena Hata msimu huu ulioisha kamecheza kwa kubembelezwa sana.Kuhusu boli kanalijua hasa pass za masafa marefu,we onesha tu unataka kaiweke wapi ,utaikuta hapo hapo ulipoomba.
 
Amesema hataki habari za mpira kwanza haupendi anacheza kama kazi
Dah! Kuna watu wamebarikiwa duniani na hawaoni kabisa maajabu ya baraka zao. Niliwahi kusoma makala ya Cadabra naye akisema kuwa haupendi mpira ila anacheza tu kama kazi! Imagine soka lilivyo na burudani halafu kuna wana wanacheza wakiwa kati ya top performers wa dunia na wala hawapendi!

Ningepewa hata 1/10 ya uwezo wa Toni ningekuwa kiherehere sana kwenye soka, nadhani dunia yote ingenijua hata kama ningekuwa ihefu.

Kweli kwenye miti hakuna wajenzi
 
Back
Top Bottom