KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Tangu Zitto Kabwe ajitoe ufahamu wa kuandika barua WB ili mkopo kwa ajili ya elimu tulioomba tusipewe, baadhi ya watu wameanza kuujadili usaliti wa Zitto Kabwe kwa Taifa lake kama uzalendo na yeye kujiona kafanya kitendo cha kishujaa kwa watanzania maskini.
Mashaka ya wengi ni kwa nini Zitto kaamua kuwa sehemu ya unyonyaji badala ya kutumia kalamu yake kulisaidia taifa lake? Zitto anajulikana kwa sifa moja kubwa nayo ni kusaka umaarufu na ukuu kwa gharama yoyote bila kujali athari kwa watu wake, kwa taifa lake na kila mmoja mwenye mapenzi mema, rejea cheo alichonacho ACT cha kiongozi mkuu wa chama ambacho kinaonesha ni mtu mwenye utu na tamaa ya ukuu na mamlaka yasiyo na mipaka.
Ninaamini Zitto ni moja ya watu wanaosubiri anguko la Rais Magufuli au serikali kwa sababu anaamini haitaji kuwa kiongozi mkuu wa chama bali kuweza kuwa hata kiongozi mkuu wa nchi ambaye hatotamani katiba na sheria imwambie nini cha kufanya Zaidi ya utashi wake binafsi. Namuona kama mtu mwenye uchu wa kutawala na si kuongoza, amekosa sifa za kuwa kiongozi Zaidi ana sifa zote za kuwa mtawala ambaye sheria na katiba ataiweka pembeni kama akipata mamlaka makubwa Zaidi.
Zitto na wapinzani wengine wanashindwa kujua kwamba watanzania kwa umoja wetu bila kujali itikadi, dini, Imani, kabila na rangi zetu tunamuona Rais Magufuli katika jicho la uchapakazi, uadilifu, uzalendo na matumaini makubwa kwa Tanzania ya kesho. Tanzania ya ndoto zetu na hatutaacha kuwa pamoja naye kwa sababu ushindi wake ni ushindi wetu na kushindwa kwake ni kushindwa kwetu, hatutakuwa tayari kuona akishindwa na hizi ndio sababu za kushinda kwa serikali ya awamu ya tano:

- Rais Magufuli anamtanguliza Mungu popote
- Wananchi tupo naye
- CCM imekuwa imara sana
- Tishio la maadui wa kupora rasilimali zetu