Kusudi la maisha (life purpose)

Kusudi la maisha (life purpose)

Izzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
553
Reaction score
1,144
Septemba 28, mwaka 2008 - Elon Musk amekaa ndani ya Control Center katika ofisi za Space X pale Hawthorne, California nchini Marekani. Hayupo comfortable kabisa - macho yake ameyaelekeza katika screen iliyopo mbele yake.

Elon Musk.jpeg


Wakati anasubiri launch ya Falcon 1, lazima atakuwa anawaza hatari iliyopo mbele yake.

Kampuni zake ziko mbioni kufilisika - wakati ambapo nchi ya Marekani inapitia anguko kubwa la kiuchumi ambalo ni baya zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu itokee 'Great Depression'; hali inayofanya mitaji iwe migumu kupatikana, na mbaya zaidi... yupo katika mchakato wa kupeana talaka na mke wake aliyezaa nae watoto watano (5).

Na kuelekea siku hii, tayari alikuwa ameshafanya launch za roketi tatu (3) mfululizo ambazo zote zilifeli, ambapo inaamanisha kama na hii itafeli, atalazimika kuifunga kampuni yake ya SpaceX. Kwa lugha nyepesi, kama akishindwa kufanya successful launch na leo tena - utakuwa ndio mwisho wa ndoto yake. Mwenyewe anasimulia kwa lugha ya kwao (Na mie sitafsiri maana sio mbobevu wa lugha);
“We were running on fumes at that point. We had virtually no money… a fourth failure would have been absolutely game over. Done.” — Elon Musk
Alikuwa ameshikwa na kihoro. Kibongo bongo tungesema - m*vi yalikuwa yanagonga chupi yake then yanarudi ndani... waliowahi kupatwa na kihoro wanaelewa. Elon Musk mwenyewe anakiri wazi;
“I never thought I was someone who could be capable of a nervous breakdown. I felt this was the closest I’ve ever come. Because it seemed pretty, pretty dark.” — Elon Musk
Mara kupitia spika inasikika sauti inasema; Lift off in 5, 4, 3, 2, 1… Elon Musk anabana pumzi...

Falcon-1-800x532.jpg


Roketi iliyopewa jina la Falcon 1 inafumuka toka kwenye uwanja wa kurushia roketi, inapaa kwa kasi kuelekea juu na inapasua anga kwa spidi kali... inakuwa roketi ya kwanza ambayo inamilikiwa na imegharamiwa na kampuni binafsi (na ambayo inatumia liquid fuel ) kufika katika Obiti!

Elon Musk II.jpeg


Kila mtu ndani ya Sapce X anaruka ruka kwa furaha, cheers zinatawala pale Control center... chupa za champagne zinafunguliwa kwa mbwembwe - wafanyakazi wanakunywa na kusherehekea ushindi!

Elon Musk III.jpeg


Siku iliyofuata, Elon Musk akiwa ofisini kwake - simu yake inaita. Anaitazama kuona nani anampigia... ni namba mpya. Anaipokea huku na kisha anasikiliza kwa makini;"Hello... "

Ni NASA na hawajampigia kumpongeza tu, bali pia wanampa mkataba wa dola bilioni 1! Kwa furaha, Elon Musk anashindwa hata kuendelea kuishika simu - anajikuta anatamka kwa sauti kubwa iliyoambatana na kicheko cha furaha,“I love you guys!”.

Elon Musk anasema; Jambo likiwa muhimu sana, lifanye, hata kama kuna kila dalili kuwa halitafanikiwa.
When something is important enough, you do it, even if the odds are not in your favor.” — Elon Musk
MSUKUMO HUU WA ELON MUSK UNATOKANA NA NINI?
Iko wazi kuwa kinachomsukuma Elon Musk sio pesa. Kama lengo lake lingekuwa ni kutengeneza mkwanja basi yeye mwenyewe anasema kuanzisha 'space company' lingekuwa ni jambo la mwisho kulifanya (Au asingefanya kabisa). Kwa mujibu wa Elon Musk, kitu kinachomsukuma ni maono yake. Anasema;
“I think it’s important to have a future that is inspiring and appealing. There has to be reasons you get up in the morning and want to live. Why do you want to live? What’s the point? What inspires you? What do you love about the future?” — Elon Musk
Kwahiyo, kusudi la maisha ya Elon Musk ni maono yake. Maono yake ni kuona siku moja binadamu tunaishi katika sayari ya Mars.

TURUDI KWA MIMI NA WEWE; TUNA KUSUDI LA MAISHA?
Na sisi tunataka kuona siku moja binadamu tunaishi katika sayari ya Mirihi? Au, tumezaliwa ili tusome chekechea, darasa la kwanza mpaka la saba, kidato cha kwanza mpaka cha nne, kidato cha tano na sita, digrii ya kwanza, tuajiriwe, tuanze kwenda kazini asubuhi mpaka jioni kwa miaka 40 au 50, tustaafu kisha tufe?

KAMA SIVYO; KUSUDI LA MAISHA NI NINI?
Kusudi la maisha ni sababu inayokufanya uamke kila inapofika asubuhi. Kusudi linaongoza maamuzi yako, lina-influence tabia yako, lina-shape malengo yako, linakupa uelekeo wa maisha na linakupa maana ya maisha. Kwa baadhi ya watu, kusudi lao la maisha lina uhusiano wa moja kwa moja na wito walionao, kazi aliyonayo inayomfanya ajisikie amani. Kwa wengine, kusudi la maisha ni majukumu waliyonayo kwa familia na marafiki. Wengine wanalitafuta kusudi la maisha kupitia imani za kiroho na kidini. Wengine wanaliona kusudi la maisha katika kila nyanja ya maisha yao.

KUSUDI LA MAISHA LINA UMUHIMU WOWOTE?
Kusudi la maisha ni hatua ya kwanza ili uweze kuishi maisha ya kueleweka. Unaweza kuwa busy kila siku, wakati huna kusudi la maisha linaloeleweka, matokeo yake unaweza kujikuta unaelekea njia isiyo yako. Kwasababu malengo yako hayaamui kusudi la maisha yako bali ni kinyume chake. Kwahiyo, unaweza kujikuta umepambana kutimiza lengo fulani kwa miaka 10, 20 au 50 ijayo, mwisho wa siku unakuja kugundua ulichokipata sicho ulichokitaka.

“If the ladder is not leaning against the right wall, every step we take just gets us to the wrong place faster.” - Stephen Covey

Wakati, ukiwa unafahamu kusudi la maisha yako ni rahisi kuweka malengo yanayoeleweka ambayo yataamua kila siku uishije. Kwa kifupi;
No purposeVague goals or no goals → Vague plans or no plans → Random daily actions, Procrastination, or Constantly busy with others’ agendas =
Clear purpose Clear goals → Clear plans → Clear daily actions =
Hakikisha ngazi yako umeiegemeza kwenye ukuta sahihi kwanza, kisha anza kupanda. Hakikisha una mtazamo mpana wa maisha yako kwanza, kisha rekebisha malengo na matendo yako ya kila siku. Mtazamo mpana wa maisha yako ndio kusudi la maisha yako.

UNAWEZAJE KUJUA KUSUDI LA MAISHA YAKO?
Zipo namna nyingi, lakini hapa nakupa namna rahisi kabisa.

TAFUTA MAJIBU YA MASWALI YAFUATAYO:
1. Ulipokuwa mtoto, experience zipi nzuri unazikumbuka? Ulikuwa unapenda zaidi kufanya nini? - Orodhesha zote.
2. Ni nani 'idol' wako kwa sasa na kwanini unavutiwa nae? - Kumbuka, ni vizuri ukavutiwa na mtu kutokana na tabia zake, maono yake na uwezo wa kumakinika kwenye jambo lake licha ya maneno maneno ya watu. Usijaribu kuwa yeye, bali jifunze kutoka kwake halafu kuwa wewe.
3. Unaamini nini na kipi ni muhimu zaidi kwako? (Core values and beliefs)
4. Unasukumwa kufanya nini katika kuisaidia jamii? Ni kwa namna gani ujuzi na elimu yako inaweza kukusaidia kutimiza hilo?
5. Unajiwekea malengo ya namna gani?
6. Ukifa, unataka ukumbukwe kwa lipi?

KISHA, ANDAA MISSION STATEMENT YAKO.
*Ntatumia Kiingereza - Na hii ni ya kwangu mimi; Tumia hii kutengeneza yako.


My personal qualities: Introvert, Intellectual, A good communicator.
My talents: Cretivity, Public speaking, Teaching, Mentoring, Leading.
The circumstances that tend to repeat in my life: Teaching others, Listening to people’s problems, working with technology.
My desires: Traveling, Being my own boss, Making a difference.

Kisha chagua kitu kimojatu cha muhimu kuliko vingine kwa kila kipengele na ujaze kwenye statement hii;

I, the Computer Virus (Weka jina lako) am designed to be an introvert (Jaza sifa yako) who can lead others (Weka kipaji chako) and I find myself working with technology (Weka jambo ambalo hujirudia kwenye maisha yako) often, because I am supposed to own my own tech conglomerate and make the difference(Weka unachotamani ukitimize kabla ya kufa).

Hongera! Tayari unalijua kusudi la maisha yako, rudia kuisoma kila siku mpaka ikae kichwani. Kisha nenda kapambane kulitimiza kwa nguvu, akili na moyo wote - na hakikisha kwa chochote unachofanya unaifanya dunia kuwa mahali bora zaidi pa kuishi.

Mimi nakutakia kila la heri!
 

Attachments

  • Mars.jpeg
    Mars.jpeg
    50.3 KB · Views: 13
tunapambana kwa sababu tunaamini ipo siku tutafanikiwa hata kama miaka itakuwa imeenda lakin odds are not in our favour Lazma tukubali
 
Nakufatilia sana kwenye posts zako, ubarikiwe Mr. [emoji120]
 
Back
Top Bottom