Kusudi la mimi kuwepo duniani ni lipi?

Kusudi la mimi kuwepo duniani ni lipi?

APPROXIMATELY

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
2,035
Reaction score
2,715
Ndugu zangu wanajamii forum,kwanza napenda kuanza na Salam ile pendwa kazi iendelee

Hili swali linaibuka kutokana na watu kujikuta ghafla tupo duniani,bila ya kikao cha makubaliano na wazazi wako wote kukuleta hapa duniani.

Basi tutaishi mwisho wa siku ghafla tutaondoka(kufa) bila ya makubaliano ya wapi tunaelekea.

Hapo ndipo linakuja swali hili 'MAISHA NI NINI',Na nani aliye nyuma yake? Je, ni MUNGU au kuna kitu kingine.swali hili alishawahi kujiuliza mfalme Suleiman mwana wa daudi,ambaye Biblia inamtaja kuwa alikuwa ni mfalme mkuu na mwenye, busara na nguvu kuliko wa falme wote na pia alikuwa tajiri kuliko matajiri wote waliokuwa kabla yake na badala yake.

Basi mfalme Suleiman akasema atajaribu kila kitu, kwanza akaanza na ELIMU.akatafuta elimu kwa bidii, akaipata akawa na elimu kubwa ya kufahamu kila mnyama, mimea na viumbe vyote duniani, na hekima iliyopo ndani ya hao wanyama, akaweza kutatua mafumbo magumu sana, akatunga mithali nyingi sana na akaandika vitabu vingi sana.

Alifanya hivyo pengine angegungua jambo fulani ambalo lingemsaidia kupata kanuni rahisi ya watu kuishi duniani au maisha ya raha,na uhuru au ya furaha, lakini alivyojaribu kufanya hivyo ndivyo hali mbaya ilizidi kuongezeka huzuni na masikitiko.

Akasema nitajaribu wanawake, akaenda kuoa wake 700 wanaotoka katika majumba ya kifalme tu, pia alioa na masuria 300, aangalie labda akiwa na hao atafanya maisha kuwa bora duniani, au furaha.

Hilo nalo halikumletea majibu aliyokuwa anatafuta..

Akajenga makasri makubwa, na kujiwekea posho kubwa ya chakula cha mwaka nzima, kila siku kwake ilikuwa ni sherehee, lakini bado hakukipata alicho kuwa anatafuta.

Akajaribu pombe, akawa anakunywa divai,lakini bado hakuna lolote aliloliona ndani yake lingeweza kufichua fumbo kubwa la maisha.

Akajaribu upumbavu na wazimu, yani mambo yote ambayo unaweza kuona ni ya kipumbavu au niya wenda wazimu, kama vile kujitukuza, pengine kucheza dansi, n.k, lakini hakuna hata moja liliweza kumpa maana ya mambo yote.

Akajaribu kuwa na malengo makubwa akawa mfanyabiashara mkubwa duniani, labda akishafanikiwa hapo atakipata kitu alichokuwa anakitafuta, lakini anasema bado hakukipata.

Ndipo katika hatua ya mwisho ya uzee wake, anagundua siri kubwa ya maisha kumbe mambo yote ni UBATILI.

Mito inapotoka ndipo huko huko inaporudi.

Jua linapochomoza ndipo huko huko litakuja kuchomoza tena.

Upepo unapovuma ndipo kule kule utakaporudi, kila kitu kipo katika mzunguko wake.

Yule MUNGU niliyeanza nae, nitakapojitaabisha kwenda mbali naye, nitakaposema simtaki tena nataka nitafute ukweli wa maisha, ndiye yule yule mwishibwa siku nitamrudia.

Anayekitengeneza kitu ndiye anayejua kusudi lake,aliyetengeneza gari,anajua kwanini alitengeneza gari.

Kama unaamini MUNGU ndie aliyekuumba na ndie ameruhusu uwepo duniani sio mtu mwingine.

MUNGU anajua unalopitia, haijalishi unapitia kipi maishani, MUNGU ana mpango wa kukutoa kwenye hicho unachokipitia, mawazo yake siku zote ni ya amani kwetu.

Kila mtu anakusudi la kuwepo duniani, hujaja duniani kutembea, kuna kitu MUNGU anataka ufanye ukiwa hapa duniani.

Kabla hujaja hapa duniani,MUNGU alikujua na ana mpango kabisa na wewe,MUNGU anasema''kabla sijakuumba katika tumbo,nalikujua na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa mataifa(yeremia 1:5).

Kuna watu walikataa tamaa ya maisha, walitafuta pesa kwa mda mrefu bila mafanikio lakini katika hatua ya mwisho wa mzee wao MUNGU aliwabariki.

Basi ndugu zangu haitakiwi kukata tamaa,unatakiwa kupambana mpaka tone la mwisho.

ONE TIME ONE FOR THE ROAD AGAIN...

Hapa kuna list ya watu waliofanikiwa wakiwa wazee sana..

1. KFC's FOUNDER,Hartland sanders alifanikiwa akiwa na miaka 74.
the-real-colonel-sanders.jpg


2. Charles Darwin alifanikiwa akiwa na miaka 50
10-things-you-may-not-know-about-charles-darwins-featured-photo.jpg
 
Inaonekana jamii forum wanapenda uzi mwepesi,usio natija juu ya maisha yao,mara kula tunda kimasihara,ila vitu vya maana hawachangii
 
Kusudi ni

Kuishi na Kufa

Umekoswa upendo?
Umekoswa amani?

Yepo mengi unayashudia.. amsha tafakari km jamii

Zepo njia mbalimbali za kukuza usawa na kua na utambuzi wa kusudi lako wewe kua hapa duniani

Nikuulize mtia mada kabla haujawa hapo ulikua wapi? Yaan kabla haujawa hapo duniani ulikua wapi?

Kwa mtia mada..
 
Back
Top Bottom