Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Wakati Taifa limeilungana kupambana na shambulio la COVID-19, vyama vya upinzani nchini wakiongozwa na CHADEMA na ACT walisusia Bunge la Bajeti kwa kisingizio wanajiweka karantini dhidi ya CORONA
Ikumbukwe kwamba viongozi na wabunge wa vyama hivyo walianzisha kampeni ya kushambulia juhudi za serikali na umma za kupambana na kuenea kwa maambukizi hayo. Wafuasi wao ndani na nje ya nchi walisimama kidete kuishambulia serikali hasa wakielekeza mashambulizi kwa rais JPM pale alipoliomba Taifa kuingia katika maombi ya siku tatu kuomba Mungu aingilie kati na kulilinda taifa dhidi ya janga la COVID 19.
Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA na kiiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni alitangaza mgomo wa Bunge na hatimaye wabunge kususia Bunge la Bajeti. Hata walipobembelezwa walijibu kwa kiburi na jeuri huku wakijiaminisha kwamba wabunge wa CCM watakufa kwa mamia kutokana na maambukizi ya Corona.
Endapo Bunge liingeingia mtego wa CHADEMA kujiweka karantini ilihali hakukuwepo na tishio dhahiri la Corona ina maana bajeti ya 2020/2021 isingepitishwa na leo tusingekuwepo na uchaguzi kwa sababu ya COROna.
1. Je kuna haja gani ya kuwaamini vyama vya upinzani ambavyo kutwa wanahangaika kuibua mitafaruku na taharuki kwenye Taifa letu,
2. CHADEMA wana uhalali gani kuomba kura zetu wakati tunajua walitukimbia wakati wa shida?
3. Mgombea wao wa urais ameonyesha dharau ya hali ya juu kwa mahakama baada ya kutohudhuria ktk kesi yake na kuidanganya kwamba anajiweka karantini ilihali alikuwa anashiriki public gatherings bila hata kuvaa barakoa na social distancing.
4. ACT kupitia kiongozi wao Zitto alijitahidi sana kuiambia dunia kwamba serikali ya Tanzania hususani JPM wanaficha taarifa za Corona na wagonjwa wanakufa hovyo mitaani.
Kwa yote hayo na mengine, vyama vya upinzani wanakosa uhalali wa kushika usukani wa maongozi ya nchi yetu.
Wananchi wanaenda kuonyesha mshikamano wao kwa Magufuli na CCM kupitia sanduku la kura hapo Oktoba 28.
Wakatabahu
Msanii JF