Kutafuta Ajira Kunavyoweza Kumuathiri Mtu Kisaikolojia!

Kutafuta Ajira Kunavyoweza Kumuathiri Mtu Kisaikolojia!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Posts
4,191
Reaction score
677
Wengi wao wamekuwa wakikumbana na vikwazo vingi na manyanyaso ambayo yamewaathiri kisaikolojia na kujikuta wakijiingiza katika tabia mbaya au kuwa watu waliochanganyikiwa akili.

Utafutaji kazi si suala jepesi katika nchi kama hii ambayo ajira ni ngumu. Hatua iliyopo sasa ni kwa vijana wengi kuona ni rahisi kusoma kuliko kupata ajira. Pengine huu ni ukweli ambao umewafikisha wengi katika tabia za ukahaba na uvutaji bangi kutokana na kukosa ajira licha ya kupata elimu.


Inahuzunisha na kukatisha tamaa pale kijana anapoingia ndani ya ofisi na kukumbana
na majibu ya hovyo kutoka kwa katibu muhtasi wa meneja aliyemwendea kuomba ajira.

Kwa mfano msomi mwenye vyeti na taaluma anapojibiwa hivi! "Aliyekuambia hapa kuna kazi nani, wee unafikiri kwa cheti chako hiki unaweza kupata kazi hapa, labda ya
kufagia.

"Kaka nimekuambia hakuna kazi hebu ondoka wapishe wenye shida za maana wamuone bosi,
unaganda kama ruba?"

Ni wazi kwamba maneno ya namna hii yanapomwingia akilini kijana huku akiwa na ufahamu kuwa kuna vijana wenzake aliokuwa akiwazidi alama shuleni wameajiriwa kwenye ofisi nyeti za serikali, itamuathiri sana kisaikolojia na kitakachotokea ni ukataji tamaa.


Pengine kwa kufahamu hilo na kuwa mmoja kati ya mshauri niliyekutana na makundi ya vijana wasomi ambao wamegeuka walevi na ombaomba, nimelazimika kuandika makala haya ili kuwaimarisha kisaikolojia.


Kwa upembuzi wangu ambao umeshibishwa na makala ya Jay Crawford wa Marekani iliyoitwa "Tips on what Not to do when seeking employiment, nimelazimika kuandika makala haya ili niwape dokezo kadhaa vijana wenzangu wanaosaka ajira. Zifuatazo ni dondoo chache za muongozo!


UCHUNGUZI NI MUHIMU


Ofisi nyingi na hasa zisizohitaji wasomi wenye taaluma zimejiwekea utaratibu wake wa kufuata katika kuwapatia kazi za muda watu. Hivyo ni muhimu kwa msaka kazi kwenye eneo la aina hiyo akafanya uchunguzi kupitia kwa rafiki zake waliomtangulia hapo, ili ajue la kufanya atakapofika kuomba nafasi ya kuwa kibarua wa wiki au siku. Hii ni kwa wale ambao hawana taaluma. Maana si busara kukurupuka na kumwingilia bosi ofisini bila kufahamu utaratibu, unaweza kufukuzwa badala ya kusikilizwa.

UTUNZE NA KUUKUZA UJUZI WAKO


Inashauriwa kuwa, mtu anapomaliza masomo na kupata taaluma yake ni bora akautunza ujuzi wake kwa kujisomea na kujikumbusha kile alichosomea. Hii itamsaidia kushinda katika usaili wakati akisaka kazi. Hivyo ni bora kwa msaka ajira kukubali kufanya kazi za muda ili kujizoeza, si busara kukaa nyumbani na vyeti ukisubiri ajira.


Fahamu kuwa wakati ukijitolea ni rahisi kufahamika na watu na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya
kupata ajira.

USITAFUTE AJIRA KWA PUPA


Watafutaji wengi wa ajira huwa na kasoro ya kufanya mambo kwa pupa, hujikuta wakikusanya nguvu nyingi kwa wakati mmoja na kukimbia huku na kule kutwa nzima kutafuta kazi. Mara nyingi watu wa aina hii huwa kama wendawazimu wakipita hata kwenye maofisi ambayo hayaajiri watu wenye taaluma zao.


Jambo hili ni baya kwani huwaondolea umakini na linachosha kwa kiasi kikubwa. Kinachotakiwa ni utulivu na ufuataji wa taratibu zilizopo za kutafuta kazi. Kwa mfano, mbali na matangazo ya kazi kutolewa kuwaruhusu watu wenye sifa kuandika barua za maombi, nchini kwetu kuna njia ya kutumia marefa ambao wamo ndani au karibu na waajiriwa. Njia hizi ni bora na zinaheshima.


Kwa mujibu wa wataalam wa masuala ya kisaikolojia watu wengi wanaofanya mambo yao
kwa pupa hukabiliwa na hatari kubwa ya kukata tamaa hasa wanapokutana na mikwamo.

Ni rahisi kwa mwenye pupa kukosa njia mbadala ya kupambana na kikwazo, kutokana na ukweli kwamba wakati akishindana katika hatua za awali alitumia kiwango kikubwa cha nguvu, hivyo anapotafakari juhudi za kuongeza hujikuta akigota katika jibu la haiwezekani kushinda.


KUBALI MATOKEO YA HASI


Watafuta kazi wengi huwa hawako tayari kukubaliana na matokeo hasi. Mara nyingi wanapojaribu na kukosa hujiona kama ni watu wenye mikosi. Lakini ukweli unabaki kuwa kuthubutu ndiyo mwanzo wa ushindi wa kila jambo.


Hivyo ni busara kujaribu kuomba kazi na kuwa tayari kupata jibu la umeshindwa. Hakuna ubaya pale mtu anapokosa baada ya kujaribu, kwani kushinda ni zao la majaribio.


USIJILINGANISHE NA WENGINE


Watu wengi wamejikuta wakiathirika kisaikoloji kutokana na kasumba ya kujilinganisha na wengine. Ni hatari kubwa kumchukua mtu uliyekuwa ukimshinda masomo darasani na kumuingiza katika kipimo chako cha kukosa! Utajikuta ukiibuka na maswali mengi
magumu, yatakayokufanya ujione kama ni mtu usiyestahili kupata mafanikio.

Siku zote unapotafuta ajira simama kama wewe hata kama umemkuta rafiki yako mbumbu akiwa ofisa, usiangalie nyuma, weka mbele bahati yako na usiilalie mlango wazi ya mwenzako
 
bravo.. tatizo lingine ni watafuta kazi kushindwa kunadi vema ujuzi na utaalam wao!?
 
Mzee hongera kwa post nzuri sana ila sikubaliani na wewe kwenye hitimisho lako umetumia neno "BAHATI" hakuna kitu bahati duniani ..........luck is when an opportunity meets the prepared mind au............when struggle meets an opportunity......siamini katika bahati kabisa nasiamini katika kuomba omba kazi naamini katika kujiajiri na kupanga Idea zangu na kutafuta watu ambao naamini wataniongoza katika kuzitekeleza.


Baadhi ya hao watu tunaowaomba kazi nao walipitia mashoruba tajwa hapo juu va majibu ya hovyo kwa hio nao they feel its ample time to practice the same.....
 
Suluhisho ni uchumi kukua kwa kasi na hivyo kuzalisha nafasi tele za ajira. Ndiyo maana ni muhimu kutumia kura zetu kuchagua serikali itakayokuwa makini na itakayoshughulikia uchumi wetu vizuri.
 
Suluhisho ni uchumi kukua kwa kasi na hivyo kuzalisha nafasi tele za ajira. Ndiyo maana ni muhimu kutumia kura zetu kuchagua serikali itakayokuwa makini na itakayoshughulikia uchumi wetu vizuri.

Sasa mkuu uchumi utakua vipi kama watu hawataki kujiajiri na wanasubiri ajira.Serikali haiwezi kuweka mazingira ya kila mtu kuajiriwa hata kama itakuwa ya Dr Slaa. Itakachofanya ni kuweka mazingira shindani, basi.Hata wanaotaka kujiajiri hawataki kufikiri, wanasubiri jamaa aanzishe biashara fulani na yeye ananzisha kilekile mahali palepale............!!!!!
 
Sasa mkuu uchumi utakua vipi kama watu hawataki kujiajiri na wanasubiri ajira.Serikali haiwezi kuweka mazingira ya kila mtu kuajiriwa hata kama itakuwa ya Dr Slaa. Itakachofanya ni kuweka mazingira shindani, basi.Hata wanaotaka kujiajiri hawataki kufikiri, wanasubiri jamaa aanzishe biashara fulani na yeye ananzisha kilekile mahali palepale............!!!!!


kuanzisha mazingira shindani, ndio challenge kwa serikali

pia kuwaandaa wanafunzi wetu kuwa na fikra za kujiajiri linahitajika

mitaala yetu tokea msingi hadi sekondari na vyuoni ijikite kwenye maeneo hayo

ni aibu lkn ni kweli hata msomi mwenye Phd hawezi kujiajiri anategemea aajiriwe hii ni aibu kwa taifa
 
chagua CCM

AJIRA KWA KILA MTANZANIA
 
watu wajifunze kujiajiri tokea wakiwa vyuo vikuu.

pia wangeanza japo na tabia ya kufanya kazi part time wakiwa vyuoni na hivyo kuweza kusoma uzuri mazingira ya kazi na nafasi wanazoweza kutumia kuandaa ajira zao.
 
Kwa wanaotegemea ajira ya kamshahara kuishi................................this is your message

"Utaendelea kuwa mtumwa siku zoooooote za maisha yako mpaka hapo utakapozinduka na kujifunza skills za kujiajiri mwenyewe. Opportunities za self employment ziko nyiiiiiiiiiiiiiiiiingiiii sana, ni ubishi tu na kutokuwa na akili za kufundishika unafanya watu wasizione. Makampuni yanauzwa na kununuliwa na kufilisika kila siku. Kwa nini uweke maisha yako kwenye mikono ya bosi wako/mwajiri wako wakati akili na nguvu unazo???"

POOR PEOPLE LOOK FOR JOBS, RICH PEOPLE BUILD NETWORKS- Robert Kiyosaki.

Amkeni!!!!
 
Back
Top Bottom