Kutafuta mchumba-feedback

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
12,576
Reaction score
14,522
WanaJF wenzangu Salamu,

Kumekuwepo na threads kadhaa za kutafuta wenza (wachumba, Marafiki, wake na waume) nafurahi wanaJf wamekuwa wakichangia kwa hali yoyote ile ili kuwafanikishia lengo mahususi wahitaji.

Lakini nilifikiri pengine kama walivyojitangaza kutafuta hao wenza basi wangerudi tena humu Jamvini na kutujulisha hata kwa senteso moja juu ya kufanikiwa au kutofanikiwa kwao.

Sina kumbukumbu sahihi kama hilo limefanyika kwa baadhi yao na hivyo Binafsi kudhani kuwa hakuna aliyefanikiwa kati ya wale waliorusha thread kuomba mahusiano hayo.

Nadhani kiungwana Kama familia Moja ingependeza Kuleta Feedback iwe ni Chanya au Hasi kitu kitakachosaidia upongezwe kama umefanikiwa au kushauriwa ujipangaje upya kama hujafanikiwa.

Naomba Kuwasilisha WanaJF wenzangu.
 
Mimi natafuta mtoto, kama kuna wanadada wa kunipa muongozo basi nikipata kitarudi jamvini
 
Mimi natafuta mtoto, kama kuna wanadada wa kunipa muongozo basi nikipata kitarudi jamvini

Anza kutafuta mwenza ndo utafute mtoto, au kaka bado una ile ya kudanganywa kwamba mtoto ananunuliwa Hospital? au kuokotwa kwenye kichuguu? Tafuta Mwenza kwanza kaka!!!
 

aaah mkuu mi mbona nilimpata Nyanzala wangu humu humu na alirudi kuwapa feedback....sasa tuko bize tutengeneza watoto na tuishi miaka 8,000
 
mimi nilikurudisha majibu kaka

hata juzi nimerudia humu........

nnilifanikiwa sana...... tuko huku ote tunabeba mabox na katoto karibia kanaanza vidudu
 
Ni kweli watuambie wamefanikiwa au hawajafanikiwa ili na wengine watangaze nia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…