#COVID19 Kutahadharisha kuhusu wimbi la tatu la Covid-19 bila kuchukua hatua stahiki ni kumpigia mbuzi gitaa

#COVID19 Kutahadharisha kuhusu wimbi la tatu la Covid-19 bila kuchukua hatua stahiki ni kumpigia mbuzi gitaa

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Kwa sasa wizara, mahospitali TVs na radio kelele ni kujikinga au kuchukua tahadhari za wimbi la tatu la Covid-19.

Lakini tahadhari hizi sioni kama zina maana yeyote kwa mwananchi sababu watu wanaendelea na maisha kama kawaida inasaidia nini? Hutoi takwimu ili watu wajue kuwa mdudu kashaingia kweli nani ataamini kuwa kuna wimbi la tatu?

Tanzania hatutaki lockdown lakini hatua zichukuliwe kwa vitendo. Kiongozi unakusanya umati kwenye ukaguzi wa miradi, watu wanabanana kwenye daladala kama kawaida, wanajazana uwanjani, wanakutana kwenye vikao, makanisani, misikitini, mashuleni hayo matangazo ni itawakinga?

Endeleeni na matangazo tu bila hatua tuone kama kuna kitakachobadilika.

Mtanzania uhai wako uko mikononi mwako mwenyewe, endelea kuzembea uone kama haujaupoteza

1. Vaa barakoa
2. Nawa mikono mara kwa mara
3. Usisongamane kwenye watu wengi

Kuvaa barakoa sio ushamba au uoga ni hekima kwako ya utambuzi
 
Shida tuliyonayo ni yale maono ya Mwedazake bado yanasumbua watendaji na raia wengi. Inabidi Serikali na taasisi zake za maswala ya afya kwa nguvu kubwa kuanza kupambana na Covid kisayansi kama tume ya mama ilivyopendekeza.

Mama alitakiwa kupiga chini watendaji wote wa waliokuwa wakiongoza hizi taasis za afya kipindi cha Mwendazake, kwani huwezi kutumia watu hao hao kutatua tatizo ambalo wao walisha sema halipo.
 
Shida tuliyonayo ni yale maono ya Mwedazake bado yanasumbua watendaji na raia wengi. Inabidi Serikali na taasis zake za maswala ya afya kwa nguvu kubwa kuanza kupambana na Covid kisayansi kama Tume ya mama ilivyopendekeza.
Kabisa mzee. Naona kama kelele tu,na kwa sasa itatuchapa sana ngoja inatuvutia kasi tu.
 
😬😁😁Wavaaji ni wachache sana ndio maana ukivaa unaonekana kama mchawi (mleta corona)

Hudhani ni mwendelezo wa mambo haya:

😬😁😁Wavaaji ni wachache sana ndio maana ukivaa unaonekana kama mchawi (mleta corona)
Siku zote kwenye maisha yako,usifanye jambo ili kufurahisha wengine au kusubiri reaction yao kwako.

Fanya jambo kama lina manufaa na wewe, jinsi watu watakavyo lichukulia hiyo wewe isikushughulishe.

Kila mtu na maisha yake na maamuzi yake ili mradi asivunje sheria za nchi tu au kwenda kinyume na maagizo ya Mungu.
 
Pana mburumundu walioaminishwa kuvaa barakoa ni ushamba.

Ngoja waje.
Dah, Mburumundu! Umenikumbusha utoto Mkuu, kuna mwanamazingaombwe mmoja alikujaga shule nikiwa darasa la kwanza ndio alikua anajiita hivyo.
 
Shida tuliyonayo ni yale maono ya Mwedazake bado yanasumbua watendaji na raia wengi. Inabidi Serikali na taasis zake za maswala ya afya kwa nguvu kubwa kuanza kupambana na Covid kisayansi kama Tume ya mama ilivyopendekeza.
Ipambane na Covid ipi? Mbona mnatafuta vitu visivyo na shida ninyi? Corona ingekuwa serious Tanzania Hali ingekuwa Kama hii?

Acheni kuiga Mambo, Corona haimalizwi kwa mbinu unazodhani vinginevyo mtapigwa lockdown mfie sebuleni.
 
Dah, Mburumundu! Umenikumbusha utoto Mkuu, kuna mwanamazingaombwe mmoja alikujaga shule nikiwa darasa la kwanza ndio alikua anajiita hivyo.
Anaweza kuwa ni mmoja wao. Rangi yao si unaitambua?
 
Fanyeni shughuli zenu acheni kurudi kwenye mtego wa huu upuuzi unaoitwa Corona, this is just a business.
Kuna mwingine hapa alikuwa na mawazo kama yako mkuu:

Wala usidhani kuwa uko peke yako.
 
Ipambane na Covid ipi? Mbona mnatafuta vitu visivyo na shida ninyi? Corona ingekuwa serious Tanzania Hali ingekuwa Kama hii?

Acheni kuiga Mambo, Corona haimalizwi kwa mbinu unazodhani vinginevyo mtapigwa lockdown mfie sebuleni.

Inasikitisha sana...
 
Duh! Mzimu wa mwendazake huu.
 
Back
Top Bottom