PreGE2025 Kutaka ichapishwe Fomu Moja 2025 kwa Mgombea wa CCM, Demokrasia imezingatiwa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakili Fatma Karume amefafanua kuwa chama chochote cha siasa kinachobinya demokrasia ndani ya chama, kwa mujibu wa aheria na mmlaka aliyonayo msajili wa vyama vingi vya siasa inabidi achukukue hatua ya kuiandikia barua kwanini chama hicho kisifutwe:

CCM HATIHATI KUFUTWA NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA, KWA KUBINYA DEMOKRASIA NDANI YA CCM KUTOKANA NA KUTOA FOMU MOJA TU YA MGOMBEA URAIS

Fatma Karume: Hatuna Utawala Wa Sheria, Tuna Watawala wa Sheria​

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na taasisi ya TWCP - Ulingo wameandaa tukio kuwakutanisha wanawake na wadau wengine kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani IWD leo Machi 8, 2024.

Fatma Karume ahoji Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kutochukua hatua pale Mwenyekiti wa CCM taifa alipopiga marufuku mikutano ya kisiasa, tamko lililokuwa kinyume na sheria ya vyama vya siasa kuwa lazima vyama vya siasa vikuze demokrasia ama sivyo vitafutiwa usajili.

Lakini cha kushangaza anaongeza wakili Fatma Karume , kuwa msajili akaufyata mkia kwa kutotoa kauli au karipio na kukiwajibisha chama cha CCM kuenda kinyume na sheria kwa kufuta mikutano siyo tu ya vyama vingine bali hata ya CCM kwa miaka 6 kinyume na sheria ya vyama vingi ambayo msimamizi wa vyama yaani Msajili wa Vyama vya Siasa anatakiwa kuhakikisha vyama vinakuza demokrasia ama sivyo anaweza kuvifuta kama sheria inavyotamka....
 
Fatma ni Mwanasheria ajue kuwa Ili aifute CCM lazima ajue ikiwa msajili anacho cheti Cha kusajiliwa CCM kama vyama vingine hapo 1992.

Wananchi tuungane kuzuia CCM isikabidhi Nchi Kwa wageni kupitia Mwenyekiti wa chama.
 
Fatma ni Mwanasheria ajue kuwa Ili aifute CCM lazima ajue ikiwa msajili anacho cheti Cha kusajiliwa CCM kama vyama vingine hapo 1992.

Wananchi tuungane kuzuia CCM isikabidhi Nchi Kwa wageni kupitia Mwenyekiti wa chama.

Msajili asisite kukichukulia hatua stahiki chama hiki kongwe kwa kubinya demokrasia na haki ya mwanachama kuchukua fomu atie nia ya kufikiriwa achaguliwe kugombea urais kwa tiketi ya CCM kwa kuchuana na mwanachama Samia Suluhu Hassan na wengine watakaojitokeza.


TOKA MAKTABA :

Msajili atakiwa kukifuta chama​

WEDNESDAY , 4TH APR , 2018
NA MELLANIA JULIUS
Kamati ya Sheria, Katiba na Utawala imemtaka msajili wa vyama vya siasa asisite kukifutia usajili chama chochote cha siasa nchini ambacho kitakiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya siasa nchini.


Picha: Mohamed Mchengerwa

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Sheria, Katiba na Utawala Mohamed Mchengerwa akiwasilisha maoni yao Bungeni, na kusema kwamba msajili wa vyama vya siasa asisite kukifutia usajili chama ambacho kitaenda kinyume.

“Kamati inashauri na kusisitiza kwamba ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ihakikishe kunakuwepo na kusimamia kwa ukaribu, kusimamia na kuchunguza sifa na mienendo ya vyama vya siasa nchini, na kwamba msajili asisite kukifutia usajili chama chochote cha siasa nchini ambacho kitakiuka sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji wa vyama vya siasa nchini”, amesema Mohamedi Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Rufiji.

Sambamba na hilo Kamati hiyo imependekeza kwamba ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inafanya ufuatiliaji na ukaguzi wa matumizi ya ruzuku kwa vyama vya siasa, na iwapo ikibainika inatumika tofauti, chama kinyimwe ruzuku
 
ZIMWI LA SHERIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA KUIBANA CCM

Sheria ya Vyama vya Siasa, Tanzania​


TANGAZO LA SERIKALI NA. 215 la tarehe 12/10/2007

SHERIA YA VYAMA VYA SIASA
(SURA YA 258)

-------------
KANUNI
(Zimetungwa chini ya fungu la 22(b))

KANUNI ZA MAADILI YA VYAMA VYA SIASA ZA
MWAKA 2007

SEHEMU YA KWANZA
UTANGULIZI

1. Kanuni hizi zinaitwa kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa Mwaka 2007 na zitaanza kutumika mara tu baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali.

2. Kanuni hizi, zitatumika Tanzania bara na vilevile Tanzania Zanzibar

3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa pale muktadha utaelekeza vinginevyo- “chama cha siasa” maana yake ni chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kwa mujibu wa Sheria.
“Msajili” maana yake ni Msajili wa Vyama vya Siasa aliyeteuliwa kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria pia itajumuisha Naibu Msajili na Msajili Msaidizi;
“Sheria” maana yake ni Sheria ya Vyama vya Siasa.

SEHEMU YA PILI
HAKI YA CHAMA

4.–(1) Kila chama cha siasa kitakuwa na haki zifuatazo-

(a) Kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi;
(b) Kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar;
(c) Kujadili na kushindanisha sera zake na zile za chama cha siasa kingine kwa lengo la kutaka kukubalika na wananchi;
(d) Kuwa na uhuru wa kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura; na
(e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa;
(2) Wakati wa uchaguzi wowote utakaoendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, kila chama cha siasa kitakuwa na haki na uhuru wa kushiriki na kushirikishwa na Tume ya Uchaguzi na au chombo chochote chenye mamlaka katika kufanya uchunguzi na kupata matokeo katika jambo au suala lolote linalohusu uchaguzi.

SEHEMU YA TATU
WAJIBU WA CHAMA

5.-(1) Kila Chama cha Siasa kitakuwa na wajibu wa kutunza maadili chini ya kanuni hizi kwa: -
(a) kukieleza kwa wanachama wake ili kuongeza uadilifu wa kisiasa ndani na nje ya chama cha siasa;
(b) kulaani, kuepukana kuchukua hatua zitakazofaa ili kuzuia au kuepusha vitendo vya vurugu, uvunjaji wa Amani au ukandamizaji wa aina yeyote ile;
(c) kutotumia vyombo vya dola kukandamiza na kutoa vitisho kwa chama cha siasa kingine kwa manufaa yake;
(d) kutotoa maneno yoyote au maandishi ambayo ni ya uongo na kuhusu mtu yeyote au chama cha siasa chochote;
(e) kufanya mkutano wa kisiasa na maandamano bila kufanya vurugu kwa mujibu wa sheria za nchi;
(f) kulaani na kupinga-
(i) vitendo vyenye kuashiria ukandamizaji;
(ii) matumizi ya lugha ya matusi
(iii) vitendo vya kibabe na vurugu
(iv) matumizi ya nguvu ili kujipatia umaarufu wa chama au sababu yeyote ile;
(f) Kuepuka kuteremsha bendera iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria, kuharibu kwa namna yeyote ile kitu chochote ambacho ni ishara au nembo inayotumiwa na chama kingine kama sehemu ya utambulisho wa chama hicho;
(g) Kuepuka kushawishi kwa kutoa rushwa kama kichocheo ili kupata upendeleo au heshima kwa nia ya kufanikisha malengo;
(h) Kuepuka kutumia mamlaka. Rsilimali za serikali, vyombo vya dola, au wadhifa wa kiserikali, kisiasa au ufadhili wa nje ama wa ndani kwa namna yeyote ile ili kukandamiza chama kingine.
(i) Kuepuka vitendo vya ubaguzi wa rika, kabila, jinsia, dini na mahali alipozaliwa mtu yeyote ikiwa ni jamii au asili Fulani kwa kufanikisha malengo ya siasa; na
(j) Kuheshimu maamuzi halali yaliyofanywa kwa pamoja na vyama vyote.
(2) Kwa kuzingatia Sheria, kila chama cha siasa kitakuwa na uhuru wa kushirikiana na chama cha siasa kingine kwa nia njema kwa ajili ya kupanga vikao, mikutano ya hadhara kwa pamoja au maandamano kwa wakati mmoja kama kwamba mambo hayo yamefanywa na chama cha siasa kimoja au bila kuvunja sheria za nchi.

SEHMU YA NNE
WAJIBU WA MSAJILI

6.-(1) ili kuhakikisha kwamba Kanuni hizi zinatekelezwa, Msajili atakuwa na wajibu wa-

(a) kusimamia maadili ya vyama vya siasa;
(b) kupoekea malalamiko yaliyowasilishw
a pande zote;
(c) kuzuia kitendo cha uvunjaji wa Kanuni za maadili kisiendelee na kukitaka chama au kumtaka kiongozi wa chama kujirekebisha; na
(d) kutoa onyo la maandishi kwa chama au kiongozi wa chama husika;
(2) Iwapo baada ya kutolewa onyo la kwanza kwa mujibu wa Kanuni (1)(d), chama cha siasa kitaendelea au kiongozi ataendelea kukiuka maadili hayo, Msajili atakemea hadharani ukiukwaji huo wa maadili.

7.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Kanuni ya 5, malalamiko dhidi ya uvunjwaji au ukiukwaji wa maadili yatapelekwa kwa maandishi kwa mtu yeyote kwa maandishi yakiwa yamesainiwa na mlalamikaji.

(2) Mara baada ya kupokea malalamiko, Msajili ataanza kufanya Uchunguzi dhidi ya chama cha siasa kinacholalamikiwa.


Imesainiwa na, EDWARD N. LOWASA
Dar es Salaam Waziri Mkuu
1 Oktoba, 2007
 
Ahsante Kwa taarifa.🙏
 
Sasa mbona na wewe ni CCM mkuu
 
TANGANYIKA nchi ya VITUKO na VIOJA
Mbowe anaambiwa na wanaccm aachie Uenyekiti badala ya Waliomchagua WanaChadema licha ya uenyekiti wake kuwa upo kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema na Msajili wa Vyama . CCM wanasema SIO DEMOKRASIA.
FOMU ya Kugombea URAIS ndani ya CCM Itatolewa MOJA TU hivyo MARUFUKU kwa Mwanaccm mwingine KUCHUKUA FOMU hiyo ni DEMOKRASIA ndani ya CCM
Ngoja Tuone labda Watanzania hatujui Tafsiri sahihi ya DEMOKRASIA
 
Mwenyekiti wao ana hofu sana. Anajua zikichapishwa hata mbili tu hatoboi
 
Asante. Wewe umeelewa vema hoja yangu. Kama saa100 akipita ndani ya chama bila kuhonga wajumbe zile hela za kuchukua fomu basi hakuna maneno. Ila tunataka wanaccm wenye kutaka kugombea au wale wanaccm wanataka wagombee urais wote wawe huru bila uoga au kikwazo kuchukua fomu.
 
Machawa a.k.a. mapanya buku watakuambia ni demokrasia!
Wanasema Eti tulimchagua 2020 kama mgombea Urais,

Ukiwauliza mgombea mwenza wa Samia 2020 alikuwa nani hutajibiwa,

Kwa kuwa sa100 alipata Urais Kwa kulokota, ni muhimu ashindanishwe na wengine ndani ya chama na nje ya chama, tupate Rais Bora.
 
Demokrasia ipi, CCM ina demokrasia yake
 
Demokrasia ipi, CCM ina demokrasia yake
Ni Kweli CCM Ina DEMOKRASIA yake,

Lakini ni Kwa Rais aliyepita katika mifumo ya chama na kupigiwa kura kama mgombea Urais na Rais.

Samia hakuwahi kupita mifumo ya ndani ya chama kama mgombea Urais Bali kama mpambe wa mgombea Urais.

Hilo lieleweke vizuri.

CCM haijawahi kufiwa na Rais aliyepo madarakani na kupitisha anaekaimu bila kufanya mchakato ndani ya chama.

DEMOKRASIA na Utaratibu ufuatwe, watu waruhusiwe kugombea nafasi ya Urais, mchujo upite.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…