Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mheshimiwa Dr. Dorothy Gwajima amesema kuwa kutakuwa na Sare ya Kitaifa tarehe 8 Machi 2025, kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani na pia;
Kabla ya tarehe 8 Machi, maadhimisho yataanza mikoani kwa kila mkoa kuandaa Sare yake ya alama ya eneo la mafanikio yake kwenye maendeleo ya wanawake mfano labda madini, kilimo, mifugo nk
Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kitaifa mkoani Arusha, kutakuwa na sare maalumu ya kitaifa ambayo itapatikana kila mkoa.
Pia soma:
Pre GE2025 - Machi 8 tunaadhimisha Siku ya Wanawake au Siku ya Samia? Picha zake kutapakaa kwenye vitenge vya maadhimisho ni ili iwe nini?
Wakuu, Hii ni kali. Yaani kila kitu sasa hivi ni Samia, Samia, Samia! Kwani kampeni zimeanza wengine hatuna taarifa? Msajili wa Vyama vya Siasa ni zaidi ya 0. Kuna maana gani ya kuwa hapo ofisini kama msumeno wako unakata sehemu moja tu wengine haufiki? Pia soma: Kutakuwa na sare ya wanawake...
Sare hiyo itakuwa ni kitenge ambacho kitakuwa na rangi mbalimbali, ambapo kila mwanamke atachagua kitakachompendeza, na kwamba rangi za kitenge hicho zinaunda Bendera ya Tanzania.
Sare hiyo itasambazwa mikoa yote nchini, na itapatikana kwa mtu anayetaka kwa shilingi elfu 25 na kutozidi shilingi elfu 30 kwa rejareja.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu ni ya kipekee, ikiwa ni mwaka wa 30 tangu safari ya Azimio la Beijing, China litolewe.
Kutakuwa na mikutano ya kimkakati ya mitandaoni ili jamii ijue mafanikio yaliyopatikana katika miaka hiyo 30.
Machi 7, 2025 kutakuwa na Usiku Maalumu wa Wanawake utakaofanyika mkoani Arusha, ambapo wanawake takribani 1,500 watashiriki.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025