Kutana na fundi mahiri wa ujenzi wa nyumba

Wakati unanitumia vipimo vya mita ulielewa ukubwa wake? Mm nilidhani wewe no mhindi na unataka kujenga Nyumba kama za India .
Kwa vipimo ulivyonipa Nyumba hiyo inaweza zidi ukubwa wa nusu kiwanja

Ndio mkuu...ni vizuri tukaonana
 
Hapo naona kama umechanganya madawa ndg yangu. Huyo jamaa ni fundi ujenzi kwa maana ya contractor na sio architect wala QS. Hizo ni kazi za watu watatu tofauti umeongelea hapo, ungeanza na kuchora ramani, then ungem-consult QS (mkadiriaji majengo) akupe makisio halafu mwisho ndio unamtafuta huyu mtoa mada kwa ajili ya kukujengea
 

Hapana, sijachanganya madawa, najua ninachoongea. Siku hizi inabidi lazima ujiongeze. Kama wewe ni fundi mzoefu na unajua unachokifanya na umekuwa ukijenga kuanzia msingi mpaka mtu anahamia utashindwaje kutoa tathimini ya nyumba. Kama wewe mjenzi unapewa ramani, unashindwa hata kutoa copy ramani hiyo ili siku mteja akiwa anatafuta ramani umtwange naye, basi utakuwa fundi wa hovyo. Ukiwahitaji watu watatu tofauti gharama zake nazo zinakuwa kubwa zaidi, sasa pesa yenyewe iko wapi sasa hivi ya kufanya hivyo, makampuni tu yanauwezo huo sisi watu binafsi. Tunahitaji three in one. Nakukabidhi kiwanja unanipatia nyumba, sio uniambie wewe hujui kupiga rangi.
 
Well said
 
pole sana ndugu yangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…