Kutana na Gazeti lililotabiri kuhusu simu kushikwa mkononi na kuwekwa kwenye mifuko

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
Kutana na Gazeti lililotabiri kuhusu simu kushikwa mkononi na kuwekwa kwenye mifuko




Nani anakumbuka kama Kuna siku itafika simu itaweza kuwekwa kwenye mifuko au kutembea nazo na kuwa sehemu ya Maisha Yetu nazani kati Yetu hakuna !!!

Lakini Kuna Gazeti moja liliweza kuchapisha makala moja kuhusu Teknolojia ya miaka mbele ilikua Mwaka 1963 ambapo makala hiyo iliweza kuelezea Utabiri wa Matumizi ya Simu kuwa itafika wakati itaweza kuwekwa mfukoni.



Kwenye gazeti ilo liliweza kuweka kichwa cha habari cha Namna hii " ‘You’ll be able to carry phone in pocket in future" hiki ndo kichwa cha habari kilichapishwa mwaka 1963 na Gazeti moja linaiwa Mansfield News ilikua Alhamisi Aprili 18 1963.

Nakala hiyo iliwataka wasomaji wanaosoma Gazeti ilo wasitarajie kuwa teknolojia hiyo itaweza kuachiwa miaka ya hivi karibu bali kifaa hicho Kiko maabara Bado. Alikuwa Frederick Hunstman, meneja wa kibiashara wa kampuni ya simu, ambaye alinukuliwa akisema, "Simu hii iko mbali sana katika siku zijazo-kibiashara".

Makala ya habari ilisomeka, “Siku moja, watu watabeba simu zao mifukoni. Hata hivyo, usitegemee kuwa itapatikana kesho. Hivi sasa, ni maendeleo ya maabara na inaweza kufanya kazi, kuruhusu mtoa huduma kupiga na kujibu simu popote alipo ilikua mwaka 1963 April 18.



Imepita zaidi ya miaka 62 sasa matumizi ya Simu yamekua sehemu moja Yetu ya Maisha ambapo inasaidia kufanya mawasiliano na kurahisisha maisha kiujumla. Gazeti ilo liliweza kuchapisha makala hiyo ikiwa na picha ya mwanamke akishika kifaa cha mawasiliano ambacho kina fanana na simu ya kisasa.

Kwa wale wasiojua simu za mkononi hazikuingia soko la biashara mpaka ilipofika mwaka 1980 ilipita miongo kadhaa baada ya makala hiyo kuchapishwa kwenye lile Gazeti. Nikola Tesla ndo alikua Mwanadamu wa kwanza kutabiri kuwa watu wote ulimwenguni wataweza kuunganishwa mara moja na teknolojia ambayo itarahisha mambo na kuwekwa mfukoni.

Ebu tuambie mara ya kwanza kumiliki simu ilikua lini na ulijisikiaje ?
 

Attachments

  • Screenshot_20250315-152945.jpg
    227.8 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…