Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
NDANI YA NYARAKA KATIKA SEFU YA ALLY SYKES KUTANA NA MAKACHERO WA DAR ES SALAAM NA MAKACHERO WA SALISBURY
Naamini msomaji wangu umeniona na kunisikia nikiwazungumza wala wazalendo saba waliolala ndani ya safe ya Ally Sykes.
Nimeeleza kuwa Ally Sykes na Denis Phombeah walikamatwa Salisbury, Southern Rhodesia wakielekea Lusaka Northern Rhodesia kuhudhuria mkutano ulioitishwa na Keneth Kaunda agenda ikiwa ukombozi wa Afrika.
Hii ilikuwa mwaka wa 1953 wako katika TAA bado hawajaunda TANU.
Ally Sykes na Denis Phomeah wakafungiwa ndani ya banda la nguruwe usiku kucha na siku ya pili wakatiwa ndani ya ndege warudi Dar es Salaam.
Kuna mambo mengi leo baada ya miaka mingi na kupata uzoefu katika shughuli hizi nimekuwa nikijiuliza mathalan vipi Waingereza walijua hili au lile na matokeo yake wazalendo fulani na fulani wakajikuta mikononi mwa Special Branch.
Ukisoma kumbukumbu za mkutano wa kuasisi chama cha TANU mwaka wa 1954 utakuta agenda mojawapo ni kuthibitisha kufukuzwa kazi Alexander Tobias kama Administrative Secretary wa TAA.
Alexander Tobias aliajiriwa kutokana na mazungumzo yaliyofanyika kati ya Abdul Sykes na Hamza Mwapachu nyumbani kwa Mwapachu Nansio, Ukerewe baada ya serikali kuwapa uhamisho viongozi wakuu wote wa TAA baada ya kuwakilisha mapendekezo ya katiba yaliyotayarishwa na TAA Political Subcommittee.
Ili ofisi iendelee kuwa na nguvu Mwapachu alipendekeza aajiriwe Administative Secretary pale TAA ashughulike na mambo ya kila siku ya chama.
Abdul aliporudi Dar es Salaam ndiyo akafanya mipango Alexander Tobias akaajiriwa kama Administative Secretary wa TAA, New Street.
Abdul Sykes hakujua kuwa alikuwa amewafungulia Special Branch mlango wa kuingia ndani ya ngome ya TAA.
Alexander Tobia alikuwa kachero ndani ya TAA.
Barua zote ziizokuwa zinatoka kwa Kaunda kuja kwa Ally Sykes Alexander Tobias akizisoma na bila shaka akiziwasilisha serikalini.
Hivi ndivyo walipofika Salisbury walale pale na siku a pili wapande ndege nyingine kuwapeleka Lusaka Ally Sykes na Denis Phombea hawakuvuka Immigration wakajikuta wametiwa mbaroni.
Walikuwa wanasubiriwa kwa hamu kubwa.
Kisa kirefu.
Ally Sykes na Denis Pombeah wakatupwa nje ya uwanja wa ndege usiku mbali na mji wa Salisbury hawana pa kwenda.
Hapo ndipo wakajikuta mikononi mwa na mtu mmoja anaitwa Charles Mzengele Mwafrika kibaraka na kachero wa Wazungu walowezi wa Southern Rhodesia.
Charles Mzengele alikuwa mmoja katika mkufu mrefu wa makachero unaotokea Dar es Salaam kwa Alexander Tobias hadi Salisbury.
Hakuna shaka kuwa mkufu huu ulikuwa unaanzia Nairobi.
Chares Mzengele ndiye aliyewachukua Ally Sykes na Denis Phombeah usiku ule na kuwafikisha kwa Mzungu akawafungia kwenye banda la nguruwe usiku kucha.
Kisa kirefu.
Asubuhi wakatiwa ndani ya ndege iliyokuwa inakwenda Blantyre, Nyasaland.
Lusaka Ally Sykes na Denis Phombeah walikwenda kuonana na James Chipembere bado wakiwa na nia na shauku kubwa ya kufika Lusaka kuhudhuria mkutano na kuonana na Kaunda.
Ushauri walipata pale Blantyre ni kuwa warejee Dar es Salaam kwa usalama wao wenyewe.
Mkasa mkubwa.
Hivi ndivyo vitu vilivyokuwa vimekaa kwa miaka mingi ndani ya safe ya Ally Sykes.
Historia hii yote ilikuwa ndani ya kichwa chake akinieleza mimi tumekaa wawili peke yetu ofisini kwake Mtaa wa Makunganya kinasa sauti changu kikizunguka taratibu.
PICHA: Kenneth David Kaunda, Ally Kleist Sykes, James Chipembere, Charles Mzengele, Harry Nkumbula, James Chipembere na Alexander Tobias.