Kutana na mapacha walioungana, wanaochangia via vya uzazi na kila mmoja anataka kuolewa

Kutana na mapacha walioungana, wanaochangia via vya uzazi na kila mmoja anataka kuolewa

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
10,904
Reaction score
26,184
Mapacha walioungana, Lupita na Carmen Andrade waliozaliwa nchini Mexico na kukulia Connecticut nchini Marekani, wamezua gumzo kubwa baada ya mmoja kati yao kueleza kwamba yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi huku mwingine akiwa ‘single’.

Kilichowashangaza wengi, ni kutokana na ukweli kwamba wawili hao, wameungana kuanzia kiunoni, lakini wanatumia miguu miwili kwa pamoja.

Carmen ndiye aliyekiri kuwa na mpenzi aliyemtaja kwa jina la Daniel ambapo ameeleza kwamba pacha wake, Lupita yeye hayupo kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Carmen ameendelea kueleza kwamba kumekuwa na changamoto nyingi zinazowakabili tangu wakiwa watoto wadogo, nakwamba jitihada za kuwatenganisha zilishindikana.

USSR
FB_IMG_1682625850789.jpg
FB_IMG_1682625860219.jpg
FB_IMG_1682625855769.jpg
 
Hapo kwenye suala la mahari hapo pakaziwe vizuri,haiwezekani mwamba aje kulipa mahali yenye Thamani ya mke mmoja,hapo jamaa yapasa alipe mahali ya wanawake wawili.

FAIDA KWA WAZAZI
Ni kuozesha watoto wote wawili kwa wakati mmoja

HASARA
Hasara moja wapo ni ya miaka mingi tu,mmoja wapo akiumwa basi mwengine nae ataumwa,au kuna shughuri hatoweza kufanya kutokana na kuumwa kwa mwenzake.

Ugomvi wa kimaslahi juu ya uzao wao,jee ni nani amebeba mimba au jee mtoto wa mama gani kati ya hao Mama wawili

Je, nani kati yake mimba itamsumbua sana kuliko mwengine

Wivu baina ya wao wenyewe hasa wawapo faragha.

Mungu ana miujiza yake.

Tunalo lishindwa yeye kwake hakuna kinacho shindikana.

Sent from my V2204 using JamiiForums mobile app
 
Jitahidi kutumia Tafsida vinginevyo Uzi wako utaonekana wa kihuni na kupoteza maana
Na sijui kwanini mods wameuachia hewani na ukakasi ulionao!!!
 
Back
Top Bottom