Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Advocate Rwankomez Bushoke Batamuzi, Mhaya wa Ruita Muleba ameenda kwenye harusi ya Muganyizi Byejumula Mulokozi, alivyotaka kuegesha gari yake ikawa hivi:-
Douglas Majwala.
- Mhaya – nionyeshe wenye Harrier wanapaki wapi?
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – lete huku nikuonyeshe. Paki palee…
- Mhaya – maweee! Wewe Tarishi! Mbona kuna Vogue na VX hapa?
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – VX ni la Mpishi wa chakula cha harusi na Vogue ni la Karani wa kitengo cha majitaka cha Manispaa. Ni watu wa kawaida tu hao usiogope.
- Mhaya – what do you mean?!
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – mimi sijui lugha wewe paki hapo.
- Mhaya – impossible kwa kweli, ebu nionyeshe wenye full-tank wanapaki wapi?
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – siyo kazi yangu kuingia kwenye matenki ya magari kujuwa kuna lita ngapi.
- Mhaya – basi nionyeshe Ma-advocate wanapaki wapi?
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – mbona tunachoshana! Au hutaki kupaki?
- Mhaya – hapana…, sikiliza…, ukichoshwa ndiyo unalipwa ujira, kazi yako ni kuchoswa, au hujui?
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – sasa nikusaidieje mpaka hapo?
- Mhaya – nionyeshe wenye Masters ya UK ya Sheria wamepaki wapi. Usinipeleke kwa mafisadi.
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – subiri hapo nikuitie Kamanda wewe.
- Mhaya – ngoja…, ngoja kwanza…, basi napaki hapahapa, lakini huko ndani ukumbini unionyeshe wanaoongea Oxford English kama mimi wamekaa wapi. Usinipeleke kwa washamba Wajaluo wanaoongea Cambridge English.
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – sihusiki ukumbini, nenda mwenyewe.
- Mhaya – waambie hao wenye VX na Vogue nitawaundia Tume ya Uchunguzi.
- Mlinzi (Bageni Bigacho) – kwenda zako, Advocate mzima unaendesha Harrier? Gari la Walimu Wakuu wa kike! Alafu unashoboka povu jiiingi hata haya huna!
Douglas Majwala.