Kutana na Perluigi Collina, Binadamu aliyefanya kazi ya Pontio Pilato ila akazipinga falsafa zake

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
Ipi hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa duniani? Hakuna anayejua jibu sahihi. Ila ipo moja tunayoweza kuitumia kama mfano, japo sina hakika kama ndiyo hukumu ya kikatili zaidi kuwahi kutolewa katika historia ya dunia, ila inafaa kuwa mfano mzuri. Ni ile ya Pontio Pilato kutoka mji wa Judea kwenda kwa Massih Issa Bin Mariam.

Watu walipompeleka nabii Issa mikononi mwake wakitaka auwawe, alisikiliza mashitaka kutoka pande zote mbili. Hakuona kosa linalomkabili nabii Issa kustahili kufa, ila kwa kuhofia kiti chake cha uongozi, alipitisha hukumu ya kifo kama walivotaka wale washitaki. Kumradhi, kama sijasimulia ipasavyo[emoji120].

Kila nikiifikiria hii habari, kichwani mwangu ananijia muitaliano Perluigi Collina. Yes, referee bora wa mwaka wa FIFA mara sita. Referee bora kuwahi kutokea katika historia ya soka. Referee pekee ambaye hadi anastaafu halaumiwi na timu yoyote kuwa aliwahi kuwaonea.

Aliwezaje? Subiri kwanza, hapa namzungumzia mtu aliyeongeza dakika 3 katika fainali ya UEFA mwaka 1999 pale Camp Nou, Manchester United wakasawazisha na kupata bao la ushindi mbele ya Bayern Munich. Collina ni mtu asiyetingwishwa.

Labda ujasiri wa maamuzi yake ulitokana na maisha aliyokulia utotoni. Si rahisi kulelewa na mama Mwalimu na baba askari alafu usiwe mtu wa sheria. Asingetetereka maamuzi Hata mbele ya watukutu akina Duncan Ferguson na Edgar Davies. Angetenga tuta akiwa anacheka halafu ukimlalamikia anakutwanga kadi akikukaripia. Yule ndiyo Perluigi Collina[emoji119].

Usidhani alikuwa hivo kwa wachezaji tu, hata waamuzi wenzake walikoma kumtambua. Kabla ya mechi angewaweka wasaidizi wake chini, awape 'tution' ya namna timu zote zinavocheza na wachezaji wakuwaangalia kwa jicho la tatu. Ndiyo maana Ronaldo De Lima alijiamini vile mbele ya wajerumani pale Korea Kusini katika fainali ya kombe la dunia 2002, alijua analindwa vilivyo.

Marehemu Steve Jobs alisema, "Njia pekee ya kufanikiwa ni kupenda unachofanya". Nadhani ndiyo maana Collina amefanikiwa. Immagine aliacha kazi ya jeshi na shahada yake ya uchumi ili akawe muamuzi
 
kaka hawa warumi kwenye soka wametisha kila upande.
makipa;buffon,luca marchegiani
mabeki;nesta,maldin,cannavaro,chiellin
viungo;gattuso,pirlo,conte,dino zoff
washambuliaji;dino baggio,inzagh,robart baggio,silvio piola,del piero
makocha;arrigo sachi,conte,capello,ancelliot,lippi
refa;collina
hatari sana hawa watu
 
Sahihi mkuu
 
NAJIBU KUHUSU HUKUMU:-
Hukumu ya kikatili kuliko zote imewahi kutolewa manzese. Kibaka alivishwa tairi na kuchomwa moto akijiona.
Majaji waliomuhukumu na kuikazia hukumu yao pia ndio mashahidi wa kesi kwa kosa alilolifanya kibaka. Haohao ndio waliendesha mashitaka na ndio walitekeleza hukumu.

Hukumu ilitekelezwa baada ya hoja za mshtakiwa (kutimua mbio) kutupiliwa mbali.
 

Scirea, Gentile, Baresi, Totti, Albertini, Zambrotta, Toldo, Peruzzi, Puol Rossi, Scilachi
 
dah! hawa warumi hatari sana kwenye haya mambo.hapo hatujamweka zola,
 
"dos2020" unanikumbushaga mbali sana kwenye michango yako,unanifurahisha hasa ubishi wa messi na ronaldo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapa patamu ila ungeanzia mbali kidogo kwa captain dino zoff nyanda huyowakati huo alinyanyua kwapa kombe la dunia 1982 wakiwa na mtu hatari poul rossi sijui kama umefanya makusudi au bahari mbaya kutojumuisha nyanda hawa angelo peruzz walter zenga na gianluca pagriuca achilia mbali mkungu wa chuma Franco baresi huyu jezi namba sita ya ac milan walimwambia hii unaondoka nayo hii basi acha wangine waendelee kuchangia niishie hapa.
 

Ni noma kabisa, yani kila safu unayoingia kuna watu unajaza debe kabisa. Yani Ma goalkeeper tu wakiwango cha juu unajaza ukumbi kabisa
 
Mauro Cammoranesi ingawa in Mrumi wa kuunga naye wamo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…