Kutana na Phil Jones, mchezaji asiyecheza Man Utd lakini hauzwi na hana mpango

Kutana na Phil Jones, mchezaji asiyecheza Man Utd lakini hauzwi na hana mpango

ESCORT 1

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2015
Posts
1,412
Reaction score
3,043
Philip Jones alisajiliwa na aliyekuwa kocha wa Man Utd, Sir Alex Ferguson mwaka 2011. Kipindi hiko akiwa kinda akichezea Blackburn Rovers.

Alitajwa kama mchezaji bora katika nafasi ya ulinzi wa kati kwa siku za usoni.

Phil Jones akaanza kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara. Nafasi yake ya kucheza ikawa shakani.

Mwaka 2013 Phil Jones na Man Utd ikatwaa taji la EPL na Sir Alex Ferguson akastaafu.

Baada ya hapo akaanza majeraha ya mara kwa mara, anacheza kidogo muda mwingi yupo nje ya uwanja.

Wakaja mabeki mbalimbali wakamkuta Phil Jones na wakaondoka wakamuacha jamaa palepale Man Utd.

Mabeki kama Marcos Rojo, Daley Blind, Eric Bailly, na wengineo wakaja Man Utd mpaka wanaondoka jama awamemuacha na hachezi.

Phil Jones amenusurika kuuzwa chini ya makocha kadhaaa kama vile, Moyes, Van Gaal, Mourinho, Ole Gunnar, Carrick, Rangnick na hata Giggs (kaimu kocha wa muda) na sasa Erik ten Hag.

Kwanini ananusurika? Kila inapofika majira ya kiangazi( wakati wa uhamisho wa dirisha kubwa la usajili ) Phil Jones yeye daima huwa ni majeruhi. Hivyo inakuwa ngumu kuuzwa kwake.

Sasa mkataba wake unaelekea ukingoni pengine anaweza akaondoka kama mchezaji huru, mara ya mwisho kuchezea Man Utd ni mwezi April mwaka jana.

Huyu ndio Legendary Phil Jones, watu mpaka washaanza kumsahau kama anachezea Man Utd😂😂
55EA4781-B457-4A6C-8D46-7ED3C2FA05F4.jpeg
 
Hahaaa alisifiwa kwa takwimu za tackling, duels amazing nakumbuka sana usajili wake
 
Wenzetu wazalendo sio kama sisi ingekuwa Tanzania ungesikia kelele tena unakuta mda mwingine mchezaji ni mzawa ila waingereza kwasababu ni kijana wao huoni wakimuandama.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom