Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
1.Anna Chapman maarufu kama Anna Kushchenko
Umri miaka 31
Alikuwa jasusi wa Russia akitafuta habari mbalimbali dhidi ya Marekani hususani shirika la ujasusi la Marekani (CIA) ambalo ofisa wake mmoja, H. Keith Melton, alimwelezea kama mwanamke hatari zaidi katika historia ya nchi hiyo.
Anasemekana pia aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kiongozi wa sasa wa Russia, Vladimir Putin, ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Russia. Anafanya nini sasa, bado haijulikani.
2.Samantha Lewthwaite maarufu kama The White Widow:
Umri 29
Alizaliwa Northern Ireland na kukulia London. Lewthwaite anatafutwa na polisi ya kimataifa si kwa tuhuma za shambulio lililofanyika miaka kadhaa kwenye kituo cha biashara jijini Nairobi, Kenya, bali kwa kuhusika na kutega bomu katika kituo cha mapumziko nchini Kenya mwaka 2011.
Aliibuka katika medani ya ugaidi mwaka 2005 akiwa mjamzito na kudaiwa mke wa Mwingereza mmoja aliyekuwa anatafutwa kwa uhalifu. Alipotea na kuibukia Kenya alipoungana na wapiganaji wa al-Shabab na mwaka alijikuta akitafutwa na vyombo vya usalama vya Kenya kwa kupanga njama za kutega mabomu sehemu mbalimbali jijini Mombasa.
Hata hivyo hakuna aliyewahi kumkamata, amekuwa akizunguka kati ya Kenya na Somalia kwa kutumia pasipoti feki.
3.Kanali Fanette Umuraza maarufu kama Number One Queen
Umri 32
Mwanamke huyo ni mtu wa pili katika madaraka akimfuatia kiongozi wa kijeshi wa Jeshi la Mapinduzi la Congo. Umuraza ameshiriki katika uhalifu mwingi wa kivita uliofanywa na kile kinachojiita kikosi cha M23.
Miongoni mwa uhalifu unaofanywa na wapiganaji wa kiume wa jeshi lake ni ubakaji, mauaji na kuwaandikisha watoto wadogo katika jeshi hilo. Yote hayo Umuraza huyatetea katika vyombo vya habari vinavyomfuata kumhoji.
4.Nisreen Mansour Al Forgani maarufu kama N/A:
Umri 21
Ameua watu kibao hususan alipokuwa katika kikosi cha mgambo wa kike cha aliyekuwa rais wa Libya, Muammar Gaddafi. Nisreen anasema alishawishiwa na ndugu yake kujiunga na kikosi hicho akisema pia amewaua maofisa wengi wa kijeshi waliokuwa wanamlazimisha kufanya yao mapenzi.
Alilikimbia jeshi hilo kwa kuruka chini kutoka ghorofa ya pili ambapo alipoanguka aliteguka mguu, lakini bado aliondoka. Akiwa amesomea udunguaji, ni lazima atakuwa anataka kulipiza kisasi kwa waliomfanyia ubaya akiwa jeshini.
5.Enedina Arellano Felix maarufu kama “La Jefa” (The Boss), “La Madrina” (The Godmother), “La Narcomami” (The Narco-Mother)
Umri 52.
Enedina, raia wa Mexico, ni “mzungu wa unga”, yaani muuza madawa ya kulevya ambaye kaka zake wote ama wamekufa au wako jela. Mwaka 2008 alitangazwa kuwa mwanamke anayeongoza duniani kwa uhalifu wa kuuza madawa ya kulevya kwa kumiliki kundi la Tijuana Cartel.
Akishirikiana na mwanaye, Fernando Sanchez Arellano, kundi hilo linateka watu katika kushinikiza biashara yake na hata kuua.