Kutana na wapenzi wawili wasioona na wakifanya kazi ya ushonaji

Kutana na wapenzi wawili wasioona na wakifanya kazi ya ushonaji

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Duniani kila mtu anapata wa kufanana naye na huu msemo kwangu mimi naendelea kuushikiria vizuri sana.

Sasa leo tujifunze kitu kupitia simulizi nzuri sana ya wanandoa hawa wawili ambao wote ni vipofu lakini wameonyeshana upendo wa kweli na kazi wanayoifanya inafanan na wanafanya kwa juhudi zote.
==========================

Wapenzi hawa… Andindilile Mwakifumbwa (52) na mkewe, Upendo Tebela (37) wameudhihirishia umma kwa mapenzi si upofu…wameamua kuishi pamoja kama mke na mume licha ya upofu walionao.

Katika maisha yao ya ndoa wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miezi 11 sasa, ambaye amepewa jina la Agape, wakirejesha shukrani kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa sasa wanajishughulisha na ushonaji wa vitu mbalimbali ili kujiingizia kipato.

 
Kwa kweli sisi watu wenye ulemavu masuala ya mahusiano huwa ni changamoto kubwa sana kwetu. bado jamii yetu ina mitazamo isiyokuwa rafiki kuhusiana na sisi. ingawaje, mabadiliko mengi yametokea kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na mchango wa elimu na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na kuingiliana kwa jamii baina ya watu kutoka eneo moja na eneo jingine.
 
Back
Top Bottom